Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Severine Lalika (kushoto) vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo ikiwa ni awamu ya pili ya ugawaji wa vitambulisho hivyo.Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt Philis Nyimbi (kushoto) vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Sengerema, Mwl. Emmanuel Kipole kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Magu, Dkt. Philemon Sengati (kushoto) vitambulisho kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Kwimba, Senyi Ngaga vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Ukerewe, Mwl. Cornel Magembe (kushoto) vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo wilayani humo.

BMG Habari

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amewaonya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wanaotumia mbinu chafu za udanganyifu ili kupatiwa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo na kisha kuvigawa kwa wafanyakazi wao.

Mongella ametoa onyo hilo mapema leo Februari 04, 2019 wakati akizungumza kwenye zoezi la kuwakabidhi Wakuu wa Wilaya vitambulisho elfu 55 ikiwa ni awamu ya pili ya zoezi hilo ambapo awamu ya kwanza Mkoa Mwanza ulipata vitambulisho elfu 25.

Amesema wale tayari wote waliohusika kwenye udanganyifu wa aina hiyo katika awamu ya kwanza ya ugawaji vitambulisho hivyo wamebainika na sheria itachukuliwa dhidi yao huku akiwa mkali kwenye suala la fedha zinazokusanywa kwenye zoezi hilo ambapo kila mfanyabiashara mdogo anachangia shilingi elfu 20 kwa mwaka ili kupata kitambulisho.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: