Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kagera, Ramadan Kambuga (aliyevaa shati ya rangi ya njano) akiwaongoza makada wenzake wa chama hicho katika ujenzi wa chumba cha darasa katika Sekondari ya Kalema Kata Buendangabo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM.
Bw. Ramadan Kambuga akipanda mti katika eneo la shule hiyo.

Na Mwandishi Wetu

WANACHAMA wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa Kushirikiana na viongozi wa chama hicho ngazi ya Wilaya Bukoba mjini mkoani Kagera wameshiriki zoezi la usombaji mawe kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha darasa katika Shule ya Sekondari ya Kalema Kata Buendangabo na kupanda miti ikiwa ni kuazimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama hicho. 

Mjumbe wa Halmashauri Kuu wa chama hicho Mkoa wa Kagera, Ramadan Kambuga (aliyevaa shati ya rangi ya njano) ambaye pia ameshiriki zoezi hilo,amesema kuwa ujenzi wa chumba hicho cha darasa ni utekelezaji wa ilani ya CCM. 

Kutokana na msongamano wa manafunzi darasani katika shule hiyo Bwana Kambuga ametoa kiasi cha shilingi laki moja ili isaidie kuongeza nguvu na kuweza kuondoa adha hiyo ambayo inawakabili wanafunzi wa shule hiyo. 

Bwana Kambuga pia amesema wao kama wadau wa maendeleo na wasimamizi wa serikali kupitia Chama cha Mapinduzi wataendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali  ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Bw. Ramadan Kambuga, akiwa na makada wenzake wakati wa ujenzi wa darasa hilo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: