Kiongozi wa Wasanii, Steve Nyerere akuongea na wanahabari kuwaelezea madhumuni ya Safari ya wasanii wote katika wote Februari 7, 2019 kutembelea mradi wa Reli ya Kisasa ya reli ya Kisasa ya Standard Gauge inayoanzia Dar es Salaam na kuelekea Morogoro. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa shirika la reli nchini (TRC) Jamila Mbarouk (kulia) akiongea na wanahabari jinsi walivyoweza kudhamini wasanii hao kutembelea Mradi wa mradi wa Reli ya Kisasa ya reli ya kisasa ya Standard Gauge inayoanzia Dar es Salaam na kuelekea Morogoro ambapo amesema kuwa wametoa nafasi hiyo ili wasanii wakienda, warudi na watoe ushuhuda wa kweli kwa wananchi maana wao ni kioo cha jamii.
Kiongozi wa Bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka ambaye ni mwakilishi wa wamiliki na wasanii wa bendi za muziki wa Dance akitoa machache mbele ya wanahabari.
Msanii wa Muziki wa Taarabu Khadija Kopa akitoa msisitizo wa wasanii kuendelea kumuunga mkono rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutangaza yale mazuri ambayo amekuwa akiyafanya katika kusukuma kurudumu la maendeleo Tanzania.

*Wasanii wapewa fursa adhim kutembelea mradi wa standard garge

Na Khadija Seif, Globu ya Jamii.

Shirika la reli nchini (TRC) limetoa nafasi kwa wasanii kutembelea mradi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge ili kujionea unavyoendelea.

Mradi huo wa reli ya Kisasa ya Standard Gauge umeanzia jijini Dar es Salaam na kuelekea Morogoro utarahishisha usafiri wa abiria na mizigo, pia inatarajia kukuza biashara kati ya Tanzania na nchi Jirani kama vile Burundi, Rwanda na DRC kwa kuwa baadaye itaendelezwa kwenda hadi nchi zote zilizoko mpakani mwa Tanzania.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mtendaji Mkuu wa shirika la reli nchini (TRC) Jamila Mbarouk amesema ni fursa adhimu kwa wasanii pamoja na waandishi wa habari kwa pamoja kupanda treni hiyo kwa lengo la kuangalia mradi huo uliweza kujengwa kwa awamu mbali mbali.

Mbarouk amesema Safari hiyo itasaidia kutangaza utalii uliopo ndani hasa kuwepo kwa treni hiyo ya umeme ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo ya tani elfu 10 huku iikiwa na spidi ya kilomita 160 kwa saa.

"Shirika la reli (TRC) limewapa kipaumbele wasanii, wachoraji, wacheza mpira, Washehereshaji (MC), Waimbaji watakuwa mabalozi wazuri katika kuutangazia umma treni hiyo kukagua Standard Garge mpya itakayotoka Dar es salaam hadi Morogoro" alisema Mbarouk.

Aidha ameeleza treni hiyo imeitengeneza kwa pesa za watanzania kutokana na kodi zilizokusanywa.

Mbarouk ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kulipa kodi ili iweze kusaidia uchumi wa Tanzania maana bila kodi hakuna maendeleo.

Kwa upande wake Msanii wa filamu nchini Steve Nyerere amepongeza uongozi wa Shirika la Reli (TRC) kwa kuwapa fursa wasanii na kutambua mchango wao katika jamii.

"Mkuu wa mkoa Paul Makonda anakaribisha kwa wote wanaohitaji mikopo aliyohaidi wakati wa Mkutano wa wasanii wote nchini kuweza kupata mkopo huo utakaowezesha kufanya kazi kwa weledi mzuri ili kukuza tasnia zote nchini." alisema Nyerere.

Ameongeza kuwa ni vyema wasanii kuendelea kutangaza mema yote yanayofanywa na rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo Watanzania kwa kuwa wao ni vioo vya jamii na wananguvu kweli kuleta mabadiriko.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: