MKuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akizungumza na wasanii mbalimbali, Wachezaji wa zamani na waandishi wa habari mara baada ya kufika katika kambi kubwa ya Soga mkoani Pwani wakati wa ziara ya kutembelea na kujionea jinsi shughuli za ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme Starndard Gauge Railway (SGR) kutoka Dar es salaam kwenda Morogoro unavyoendelea.


Wakiongeza katika ziara hiyo wasanii mbalimbali wamesifu juhudi za sreikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2015-2020 kwa jinsi inavyotekelezwa na serikali kwa kasi kubwa na kuleta matumaini kwa watanzania.

Mradi huo unajengwa na kampuni ya Yapi Merkezi kutoka nchini Uturuki na kwa sasa ujenzi huo umefikia asilimia 42 ambapo kazi mbalimbali zinaendelea kama vile kujenga madaraja, kupasua miamba ya milima kuunganisha tuta katika vipande mbalimbali, kutandika mataruma na reli na kusimika pia nguzo za umeme katika maeneo ambayo tayari yameshatandikwa reli.

MKuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli (TRC)Bw. Masanja Kadogosa wakati akitoa maelezo mbalimbali kwa wasanii mbalimbali waliotembelea mradi huo.
Baadhi ya wasanii wakiwa katika eneo la Soga.
MKuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli (TRC)Bw. Masanja Kadogosa wakizungumza na waandishi wa habari mbalimbali ndani ya treni.
Irene Uwoya pamoja na mwenzake wakiwa wameketi kwenye reli ya kisasa ya umeme SGR baada ya kufika eneo la Soga mkoani Pwani.
Ujenzi wa madaraja ukiendelea.
Mratibu wa ziara hiyo mchekeshaji Steve Nyerere akizungumza jambo na mwigizaji Irene Uwoya.
Mitambo mbalimbali inayotumika katika ujenzi huo.
Mataruma yakiwa tayari kwa ajili ya kupangwa kwenye tuta ili kutandika reli.
Baadhi ya maeneo yakiwa yamesimikwa nguzo za umeme.
Hii ndiyo treni ya Delux ya TRC iliyowachukuwa wasanii mbalimbali pamoja na waandishi wa habari kwa ajili ya kutembelea mradi huo.
MKuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli (TRC)Bw. Masanja Kadogosa wakimsikiliza Babu Tale Meneja wa WCB wakati akizungumza katika kambi ya Soga mkoani Pwani.
Wasanii mbalimbali wakiwa katika kambi ya Soga.
Wasanii Mchizi Mox kushoto na Mtunis ambaye ni muigizaji wa filamu wakipozi kwa picha,
Waigizaji Welu kushoto na Maya wakipozi kwa picha.
Meneja Msoko wa shirika la bima la taifa NIC Elisante Maleko akionyesha reli ya kisasa ya umeme SGR kipande kilichokamilika Shirika la bima la NIC ndilo limeikatia bima kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga mradi huo.
Meneja Msoko wa shirika la bima la taifa NIC Elisante Maleko akiwa pamoja na wafanyakazi wenzake kutoka NIC.
MKuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli (TRC)Bw. Masanja Kadogosa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii katika kambi kubwa ya Soga mkoani Pwani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: