Balozi wa Tanzania nchini India anayewakilisha pia nchini Bangladesh, Mhe. Baraka Luvanda akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Bangladesh, Mhe. Md. Abdul Hamid katika hafla iliyofanyika hivi karibuni katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Dhaka.
Mhe. Balozi Luvanda akizungumza na Mhe. Rais Md. Abdul Hamid mara baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais huyo.
Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Rais Md. Abdul Hamid mara baada ya mazungumzo baina yao.
Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Rais Md. Abdul Hamid mara baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho. Kushoto ni Dkt. Kheri Goloka, Afisa wa Ubalozi wa Tanzania ambaye alifuatana na Balozi Luvanda kwenye hafla hiyo.
Mhe. Balozi Luvanda akiwa mbele ya gwaride la heshima mara baada ya kuwasili Ikulu ya Dhaka, Bangladesh
Mhe. Balozi Luvanda akipita katikati ya gwaride la heshima mara baada ya kuwasilis Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha hati za utambulisho
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: