Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimkabidhi Kijana Hamis kiasi cha Shilingi Laki Tano kwa ajili ya Kununua chakula kwa siku atakazokuwa Hospitalini
Mkuu wa idara ya upasuaji hospital ya taifa Muhimbili Dk.Ibrahim nkoma akitoa ufafanuzi tatizo linamsumbua mtoto huyo kwa RC Makonda jijini Dar es salaam.
---
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amemtembelea na kumjulua hali kijana Hamis Hashim alielazwa katika Hospital ya Taifa Muhimbili akisumbuliwa na tatizo la Miguu kuvimba hadi kuzidi uzito wa mwili ambapo ameahidi kusaidia gharama za matibabu iwe ndani au nje ya nchi hadi atakapopona.

RC Makonda baada kuona taarifa za kijana Hamis kapitia mitandao ya kijamii aliguswa na kuona anao wajibu wa kumsaidia ambapo juzi aliagiza apelekwe hospital ya Muhimbili kwaajili ya kuchukuliwa vipimo ambapo licha ya Hamis kuugua pia anaishi katika Familia ya hali ya chini akimtegemea Mama mzazi ambae nae hana kazi baada ya Baba mzazi kufariki.

Aidha RC Makonda amesema kwa sasa hali ya Afya ya Hamis inaendelea vizuri baada ya madaktari bingwa wa Muhimbili kuendelea kuchukuwa vipimo kwa umakini wa hali ya juu.

Pamoja na hayo RC Makonda amemkabidhi Kijana Hamis kiasi cha Shilingi Laki Tano kwaajili ya Kununua chakula kwa siku atakazokuwa Hospital.

Kwa upande wake Hamis Hashim amemshukuru RC Makonda kwa moyo wa huruma aliokuwa nao ambapo ameeleza kuwa amekuwa anaishi maisha ya tabu lakini kwa sasa anajisikia faraja kuona RC Makonda ameahidi kumsaidia kwa kila jambo.

Kwa Mujibu wa Dr. Ibrahim Nkoma ambae ni Mkuu wa idara ya upasuaji hospital ya taifa Muhimbili anasema Hamis Hashim anasumbuliwa na tatizo la neva za fahamu kukuwa kupita uwezo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: