Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya tukio la kihistoria la uzinduzi wa Kampeni ya kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na kukabidhi hundi ya Shilingi Bilioni 3 alizotoa Rais Dkt.John Magufuli kwaajili ya ujenzi wa Hospital za Wilaya ya Kigamboni na Ilala eneo la Kivule ambapo ametoa muda wa Miezi 3 kuhakikisha ujenzi umekamilika.

Akizungumza katika Uzinduzi huo RC Makonda amesema serikali imejidhatiti kuhakikisha inapunguza na ikiwezekana kumaliza kabisa vifo vya Mama na Mtoto kwa kujenga Hospital za kutosha, Zahanati, Vituo vya Afya, Ununuzi wa Magari ya kubebea Wagonjwa pamoja na vifaa tiba ili wananchi wasipate tabu.
RC Makonda amesema katika Fedha hizo Wilaya ya Kigamboni imepokea Shilingi Bilion 1.5 na Ilala Bilioni 1.5 ambapo Hospital zitakazojengwa zitakuwa na watumishi zaidi ya 500 na kuongeza kuwa mbali na Ujenzi wa Hospital hizo za Wilaya pia Serikali inaendelea na ujenzi wa Hospital nyingine ya kisasa eneo la Mabwepande.

Aidha RC Makonda amewataka wanaume kuwasindikiza wake zao Clinic ili kujua maendeleo ya Afya zao jambo litakalosaidia kuepusha vifo vya mama au mtoto wakati wa kujifungua.

Pamoja na hayo RC Makonda amewataka mabinti kuhakikisha wanaepuka Mimba za utotoni ambazo zimekuwa chanzo cha ongezeko la vifo na hata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Uzinduzi wa Kampeni ya kuzuia Vifo vitokanavyo na Uzazi JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA inaenda na kaulimbiu isemayo kila mmoja anao wajibu wa kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi "MANENO BASI SASA NI VITENDO"
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: