Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akifanyiwa maombi.

Mchungaji Kiongozi Dk Getrude Lwakatare almaarufu Mama Lwakatare wa Kanisa la Mlima wa Moto Assemblies of God la Mikocheni B jijini Dar na wachungaji wenzake, usiku wa kuamkia jana, waliguswa na uongozi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kisha kumuombea ili kumuimarisha katika uongozi wake na kumkinga na maadui.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza jambo.

Tukio hilo lilijiri kanisani hapo ambapo mama Lwakatare alimwita mbele Makonda kisha kuwaita wachungaji wenzake na kumfanyia maombi hayo.
Maombi maalum yakiendelea.

Baada ya kumwita mbele, Mama Lwakatare na kanisa lote lilimwangushia maombi mazito Makonda kutokana na kazi ngumu anayoifanya katika jamii kama kupambana na madawa ya kulevya, rushwa, kusaidia kina mama na watoto waliotelekezwa na mengine mengi.

Tukio hilo lilijiri kwenye usiku wa wanandoa ambapo waimbaji kama Bahati Bukuku na Christina Shusho walipamba kwa burudani ya nyimbo za Injili.
Baadhi ya ndoa 5 za mfano zikikata keki maalum iliyokuwa imeandaliwa.

Baadhi ya ndoa 5 za mfano zikikata keki maalum iliyokuwa imeandaliwa.
Baadhi ya wanandoa wakikata keki maalum.
Mchungaji Kiongozi Dk Getrude Lwakatare, wa Kanisa la Mlima wa Moto ‘Assemblies of God’ akiendesha maombi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: