*Shirika la Ndege nalo laanza ujenzi wa uwanja unaohamishika

* Wageni wakijionea jinsi usafiri wa anga utakavyokuwa

Shirika la Ndege la Emirates, Mshirika Mkubwa na Mdhamini Rasmi wa Mashirika ya Ndege kwa Expo 2020 Dubai, leo wamezindua rasmi ubunifu wa mchoro na vile wageni watakavyojionea mambo kwenye maonesho hayo makubwa ya miezi sita.

Ubunifu huo unalenga kwamba viwanja vya maonesho hayo vya Emirates vitatumia teknolojia ya mwingiliano na ubunifu wa kutazama juu ya biashara ya wakati ujao ya usafiri wa anga. Tayari Emirates wameanza kazi kwenye viwanja husika kwa ujenzi ulioanza Machi 2019.

Mkuu Sheikh Ahmed bin Saeed Al Maktoum, Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Emirates Airline & Group alikuwa na haya ya kusema: “Kwa hakika tunaona fahari kuzindua mipango ya awali ya Uwanja wa Maonesho wa Emirates leo utakaotumika kwa ajili ya maadhimisho kwa maudhui ya Expo 2020 Dubai.

Madhumuni ya viwanja vyetu yanaendana na hayo ya Expo 2020 Dubai, kuchechemua maunganisho, kujenga uzoefu na kukuza ubunifu na uvumbuzi, kuhamasisha kujituma kwa ajili ya hatima bora. Uzoefu huu wa kuona mbele zaidi utawezesha kuonesha makubwa yanayotarajiwa kuja siku zijazo na utakuwa jukwaa kuonesha umuhimu wa hamasa kwa dunia ya leo na baadaye.

“Emirates na washirika wengine wa karibu hapa UAE watashiriki kwa kiasi kikubwa katika kutoa muunganisho kwa ajili ya mafanikio ya Expo 2020, na athari ya kiuchumi kwenye usafirishaji, sekta za utalii na ukarimu zitakazochangia AED 16.4 bilioni kwa uchumi wa UAE, ikionesha umuhimu wa sekta hizi katika kuongeza thamani ya uchumi kwa kuwaleta watu pamoja na kifungua mipaka,” akasema Sheikh Maktoum.

Mheshimiwa Reem Al Hashimy, Waziri wa Nchi, Ushirikiano wa Kimataifa wa UAE na Mkurugenzi Mkuu wa Bureau Expo Dubai 2020 naye akasema: “Tumesisimkwa kuileta dunia yote pamoja na kupata uzoefu katika tukio hili kubwa. Kwa miaka karibu 170, Expos za Dunia zimeunganisha watu katika moyo wa hamasa na furaha kwa ajili ya muda ujao, na zimeshangaza juu ya habari ya ubunifu, uvumbuzi, utamaduni, sanaa, vyakula na burudani.

“Usafiri wa anga umebadilisha uwezo wa watu kupata uzoefu juu ya kila kitu ambacho ulimwengu unaweza kutoa. Expo 2020 na Emirates kama washirika wetu rasmi wa usafiri wa anga, tutawaleta watu pamoja na katika sehemu moja, Dubai, 2020. Na viwanja vya maonesho vya Emirates vitatoa simulizi ya ajabu kuhusu majukumu ya ambayo usafiri wa anga utaendelea kuchukua na kubadilisha mambo katika nyakati zijazo.”

Maonesho hayo yatakayofanyika kuanzia Oktoba 20, 2020 hadi Aprili 10, 2021, Expo Dubai ni maonesho ambayo mmoja hatakiwi kukosa kwa sababu yatakuwa na mambo makubwa, kukiwa na mabanda ya nchi 190 lakini pia na ratiba kubwa ya masuala ya burudani, ikiwa ni pamoja na matukio mubashara ya kila siku kama vile maandamano, muziki na hafla za kitamaduni, mazungumzo yenye uhamasisho, warsha na mengine zaidi. Wapenda vyakula watakaokuwa wakitafuta dhana mpya juu ya ubunifu wa vyakula watapata fursa ya kuona na kujaribu sampuli tofauti kutoka kila kona ya dunia, kukiwapo zaidi ya aina 200 za vyakula lakini pia aina 34 ambazo hazikupata kuonekana kabla ya tukio hili la Dubai.

Uwanja wa Emirates

Ukiwa unaongozwa na dhana tatu za Expo 2020 Dubai: uhamaji, fursa na uendelevu, Uwanja wa Maonesho wa Emirates ulibuniwa kwa ajili ya kutoa taswira ya aina tofauti ambazo mashirika ya ndege yanaweza kuchukua kimfumo. Aina 26 ubunifu wa michoro ya gange za mapezi zitakuwa kwenye banda la Emirates na patakuwa na ukubwa wa zaidi ya meta 800 za nuru za LED kuweka hisia za aina yake katika mienendo kwenye maeneo husika.

Vipengele vya teknolojia ya utengenezaji wa karibuni kabisa, teknolojia za ujenzi na michoro ya ubunifu endelevu vitazingatiwa, kama vile miunganisho ya nishati ya Jua, ujenzi wa kudumu wa tovuti, uwezeshaji wa kuweka vivuli na mazingira mazuri ya ndani na nje ya Banda la Emirates.

Muundombinu huo wenye ukubwa wa meta za mraba 3,300 katika ghorofa tatu utakuwa karibu kabisa na Banda la UAE, kwa maana ya umbali wa kutembea kwa miguu tuu kutoka Banda la Al Wasl Pavilion, ambako ndio katikati ya eneo la Expo 2020 Dubai. Uwanja au banda la Emirates litakuwa na uwezo wa kupokea wageni 56,000 kwa wakati mmoja wakati huo wa Expo 2020 Dubai.

Uzoefu kwa Wageni

Banda la Emirates litatoa mwanga juu ya jinsi ya mabadiliko ya kibiashara kwenye masuala ya usafiri wa anga na kusaidia katika kusukuma mbele mjadala juu ya nguvu ya uhamaji na uhamasishaji pamoja na maendeleo yake angani na ardhini, ambayo hatimaye huwezesha muunganiko wa kifizikia kwa watu, bidhaa na huduma kote duniani katika mazingira ya kisasa, ufanisi na yenye kukuza uendelevu katika uhifadhi wa mazingira.

Ndani ya eneo hilo la Emirates kutakuwapo na mpango uliozungukwa katika ghorofa ya kwanza unaowezesha mwanga wa mchana kuingia kwenye eneo na kupunguza matumizi ya nishati. Maudhui zoefu yatakuwa kipaumbele na kuwezesha mwingiliano muda wote wa ziara kwa maonesho hayo.

Ghorofa ya pili ya jengo la Emirates litakuwa na bwalo kwa ajili ya vipindi vya wazungumzaji lakini pia na matumio ya kisekta, wakati ghorofa ya tatu itakuwa na bustani ya anga kwa ajili ya kuwezesha wageni kufurahia mazingira halisi, ukijani na maeneo wazi.

Banda la Emirates litasaidia katika kutoa simulizi ya jinsi biashara ya usafiri wa anga inavyoweza kuonekana kwa siku zijazo – kupitia mada kama vile za sayansi ya urushaji ndege, maendeleo kwenye teknolojia za injini, jitihada za binadamu kwenye sayansi na uhandisi wa urushaji ndege, upunguzaji wa matumizi ya mafuta, uvumbuzi katika uboreshaji wa mwonekano wa ndani ya ndege, ukilenga katika kuhakikisha abiria wanakuwa katika hali njema na kustarehe lakini pia hatima ya siku zijazo kwa uzoefu wa abiria kwenye viwanja vya ndege.

Kwa kutumia kanuni za msingi za tabia za mwenendo na nguvu nne za urukaji (lifti, ukokotaji, uzito na msukumo) wageni wataweza kuelewa sayansi inayotumika kwenye masuala ya urushaji ndege na kujifunza juu ya kanuni za msingi za usafiri wa anga. Watajua pia ni kwa haraka kiasi gani maendeleo ya teknolojia yatakavyobadilisha mambo.

Je, hatima ya injini itakuwa ya umeme? Hili ni moja ya maswali yatakayotazamwa wakati huo kwani wageni watakuwa wakijifunza juu ya maendeleo yaliyofanywa na yatakayofanywa katika nguvu za injini na mipango iliyopo kwa ajili ya kizazi kijacho cha ndege na pia mipango ya kupunguza uchafuzi wa mazingira.

Maabara zijazo zitakuwa zinaangalia katika uvumbuzi wa vifaa vya chuma na vile vinavyoundwa na muunganiko wa vifaa vya aina nyingi. Lengo kubwa litakuwa kutazama juu ya umuhimu wa kuwa na vifaa vyenye uzito mdogo lakini vyenye nguvu na kuepuka kutu kwa ajili ya kuwezesha matumizi bora kiuchumi katika mafuta.

Mwonekano wa ndege za kesho utasaidia wageni kushuhudia na kufurahia mabadiliko ndani ya ndege, iwe ni katika maboresho ya teknolojia kiubunifu au matumizi tofauti ya vifaa, lengo litakuwa ni kuhakikisha abiria wanakuwa katika hali njema, ikiwa ni pamoja na mpangilio tofauti wa namna ya viti na ukaaji kwenye ndege na si ajabu siku zijazo ndege nyingine zikawa hazina madirisha.

Hatimaye, wageni kwenye maonesho hayo watapewa changamoto za kufikiria, kubuni na kutoa mawazo juu ya wanavyofikiri ndege zijazo na usafri wa anga ujao uwe namna gani, kwa kuchanganya teknolojia zitakazokuwa zimechaguliwa na mapendekezo binafsi ya wahusika kwenye ndege kwa ujumla, injini na mamb mengine yanayoweza kuwa yanafafanua uzoefu wao binafsi.

Inakadiriwa kwamba asilimia70 ya wageni kwenye Expo 2020 Dubai watasafiri na kufika kwenye maonesho haya kutoka katika nchi nyingine kwa ajili ya tukio hili la miezi sita na mtandao wa Emirates wa kuwa na vituo vya kurukia na kutua 158 katika nchi 86 utasaidia sana kwenye usafiri wao na kuwa msaada mkubwa kwa Expo kuleta ziara milioni 25. Zaidi ya nchi 192 zimethibitisha kushiriki kwenye Expo 2020, ambapo Emirates watawezesha muunganiko wa usafiri wa moja kwa moja kwa nchi 67 kati ya washiriki. Shirika linaendelea kutathmini fursa kwa ajili ya huduma mpya za ndege kwa maana ya kuruka viwanja zaidi. Emirates pia wanawekeza kwenye teknolojia ya biemotri kuwezesha mfumo rahisi kwa abiria ardhini watakapokuwa Dubai. Mengi zaidi yatafanywa katika miaka ijayo kwa ajili ya kuunganisha zaidi watu na huduma.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: