Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella jumamosi Aprili 27, 2019 amemwakilisha Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya CCM Taifa, Mizengo Peter Kayanza Pinda kwenye harambee katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Yohana wilayani Sengerema.

Harambee hiyo imelenga kukusanya fedha kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya muziki vya kwaya ya “New Life” ya kanisa hilo linaloongozwa na Mchungaji Leonard Giligwa pamoja na gari kwa ajili ya Parishi ya Bomani wilayani humo ambapo zaidi ya shilingi milioni 20 zimepatikana ikiwa ni fedha taslimu pamoja na ahadi.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mchungaji wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Yohana Sengerema, Leonard Giligwa (kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) picha maalum ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya CCM Taifa, Mizengo Peter Kayanza Pinda kwenye harambee hiyo ambapo Pinda alikuwa mgeni rasmi na akawakilishwa na Mongella.
Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella, Mchungaji wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Yohana Sengerema Leonard Giligwa, Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi pamoja na Mkuu wa Wilaya Ukerewe Colonel Magembe wakiwa kwenye harambee hiyo.
Mlezi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Lweru, Askofu Godfrey Mbelwa akiwa kwenye harambee hiyo.

Baadhi ya washirika na wananchi waliohudhuria harambee hiyo.

Tazama Video hapa chini

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: