Rais John Magufuli (kushoto), Bakozi wa Sweden nchini, Mhe.Anders Sjoberg na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani. wakimsikiliza Meneja wa Mradi wa umeme wa 220kV, Makambako-Songea Mhandisi Didas Lyamuya
Rais Magufuli akimpongeza Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani wakati wa hafla hiyo.
Rais Dkt. John Magufuli akimpongeza balozi wa Sweden nchini, Mhe.Anders Sjoberg
Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akitoa hotuba yake
Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akitoa hotuba yake
Waziri Dkt. Medard Kalemani akitoa hotuba yake.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi, akitoa hotuba yake.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amezindua mradi wa ujenzi wa njia kuu ya umeme wa Kv220 Makambako-Songea na vituo vya kupoza na kusambaza umeme nje kidogo ya Halmashauri ya mji wa Songea Aprili 6, 2019.

Katika hotuba yake Rais Magufuli ameipongeza Wizara ya Nishati kwa kukamilisha mradi huo ambao utakuwa na manufaa makubwa kwa wakazi wa mikoa ya Nkombe na Ruvuma lakini Watanzania wote kwa ujumla.

“Mradi huu umeokoa shilingi Bilioni 9.8 ambazo zilikuwa zikitumika kununulia mafuta ya kuendesha jenereta za kufua umeme”. Alisema

Rais alisema mradi umegharimu shilingi bilioni 216 kati ya hizo shilingi bilioni 45 zimetolewa na walipa kodi wa Tanzania na zilizosalia zimetolewa kwa ufadhili wa Serikali ya Sweden.

Akifafanua zaidi Rais alisema, vijiji zaidi ya 122 vinavyopitiwa na mradi huu vitafaidika na umeme, vitapatiwa umemena hivyo kuondoa tishio la matumizi ya misiytu kama nishati.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alisema Kulikuwa na kazi ya kujenga njai za kusafirisha umemehuu mkubwa wa kilovolti 220 umbali wa kilomita 250 ukitokea Makambako, Madaba hadi Songea mjini.

Mradi utawaunganishia umeme wateja 22,700 katika vijiji unakopita na tayari vijiji 110 vimeunganishwa huku Taasisi za umma 114 na kazi ya usambazaji inaendelea.

Aidha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi alisema, mradi umetekelzwa kwa kioindi cha miaka miwili (2) hadi kukamilika.

“Nia ya Serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli ni kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo 2023, na hatuwezi kufika kwenye uchumi wa kati bila ya kuwa na umeme wa uhakika, sisi TANESCO tunawezeshwa kwa miradi mbalimbali mikubwa ikiwemo ule wa Rufiji Hydro Power utakaoongeza Megawati 2115 zitakazoingizwa kwenye Gridi ya Taifa.” Alisema.

Alitoa rai kuwa watanzania hawana budi kufikiria uanzishaji viwanda na si lazima view vikubwa bali hata vidogo vitaleta faida ya kuwa na umeme huu wa uhakika
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: