My brother @jaguarkenya sijui nianzie wapi lakini matamshi yako ya jana hayakuleta shangwe kamwe. Maana ya kiongozi ni kuwaongoza watu wako kwa njia mwafaka na sio vita au uchonganishi hasa hasa kwa majirani zetu Tanzania na Uganda.
Sisi wote tunatafuta riziki duniani ili tuweze kulisha familia zetu na kujenga nchi yetu. Kuna wakenya wanatafuta riziki kwa nchi zingine mbali na Kenya so uamuzi wako wa kuipa serikali masaa ishirini na nne kuwatoa wafanyikazi wenye biashara zao ambao sio wakenya ulichemsha.
Anyway nakuombea Mungu akupe nguvu ili uweze kuwa kiongozi wa maendeleo. #Rapcellency
Toa Maoni Yako:
0 comments: