Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Msanii Pierre Liquid kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 19, 2019. Wa pili kulia ni Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Mhandisi Ramo Makani. Pierre anatarajiwa kuwemo kwenye msafara wa wabunge wanaokwenda nchini Misri kuishangilia timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars inayoshiriki michuano ya kombe la Afrika nchini humo (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Amina Makilagi, Bungeni jijini Dodoma Juni 19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Chato na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Bungeni jijini Dodoma Juni 19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Rukia Kassim Ahmed, Bungeni jijini Dodoma, Juni 19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia) akijadili jambo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto) na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Faustine Ndugulile (katikati), Bungeni jijini Dodoma Juni 19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Namtumbo Mhandisi Edwin Ngonyani kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa zamani wa Namtumbo, Vita Kawawa kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni19, 2019. Katikati ni Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: