Watoto wa vituo mbalimbali kumi vya kulelea watoto wenye uhitaji mkoani Dodoma, wakipata futari iliyoandaliwa na Kampuni ya QNET jana. Hafla hiyo ilihudhuriwa na zaidi ya watoto 200 kutoka vituo hivyo na kuongozwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Mustapha Shaaban, Wawakilishi wa QNET na wawakilishi toka Bakwata.
Watoto kutoka vituo mbalimbali kumi vya kulelea watoto wenye uhitaji mkoani Dodoma wakisherehekea na Mshauri wa QNET Tanzania, Edward Mkony.
QNET, kampuni ya biashara ya mtandao duniani, sambamba na tamaduni zake na jitihada za kusaidia jamii, kusambaza upendo, huruma na ukaribu kwa kutoa msaada na kuleta faraja kwa jamii nyingi zisizo na uwezo barani Afrika. Katika zoezi ambalo lilifanyika katika nchi zote ambako kampuni hii inaendesha shughuli zake barani Afrika, QNET sambamba na wawakilishi wake wa kujitegemea (IRs), mawakala na wafanyakazi imeleta faraja, tumaini na tabasamu kwenye nyuso za wengi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kampuni ya QNET inaendeshwa na falsafa ya RYTHM - Jiinue Kusaidia Wanadamu ('Raise Yourself to Help Mankind’) imeandaa kampeni hii ya mwaka kusaidia kuboresha maisha ya familia na watoto wengi wasio na uwezo kwa kuwapatia mahitaji muhimu kama vile chakula, vinywaji na msaada wa kifedha kwa madhumuni ya elimu na kibinadamu.

Hafla ya Futari Jijini Dodoma imewaleta pamoja zaidi ya watoto yatima 200 kutoka katika wilaya kumi za mkoa huo. Pamoja na hafla hiyo ya Iftar kampuni ya QNET imetoa zawadi za mbuzi, kilo 100 za mchele, kilo 50 za unga, kilo 25 za maharage, kilo 25 za sukari na lita 20 za mafuta ya kula kwa kila vituo kumi vya watoto yatima mkoani humo.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Shaaban alitoa wito wa amani na kuihamasisha jamii kuiga mfano uliofanywa na QNET katika kusherehekea mwezi mtukufu wa Ramadhani. Sheikh Shaaban ameipongeza kampuni ya QNET kwa kutayarisha Iftar kwa vituo vya watoto yatima Jijini Dodoma, chaguo ambayo inaunga mkono mkakati wa serikali ya kuhamisha makao yake Jijini humo. Pia alishukuru kampuni ya QNET kwa moyo wa msaada na ushirikiano hasa katika mwezi huu wa Ramadhan.

Akiongea katika hafla hiyo, mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi Mwanahamisi Mukunda alisema ‘Tendo hili la Iftar imesaidia serikali ya mkoa katika utekelezaji wa majukuku yake pamoja na kuwaangalia watoto yatima’.

Hafla ya Iftar Jijini Dodoma iliudhuriwa pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Dodoma, wawakilishi wa baraza la kislamu Tanzania-BAKWATA, viongozi wa dini la kislamu wa mkoa pamoja na wawakilishi wa kampuni ya QNET.

Katika nchi za Senegali, Cameroon, Kenya, Niger, Mali, Burkina Faso, Togo, Guinea, Ivory Coast na Ghana, QNET imetoa magunia ya mchele, magaloni ya mafuta ya mboga, vinywaji baridi, vifaa vya usafi na fedha taslimu kwa yatima, jamii za waisiliamu, vituo vya kutoa msaada wa kielimu na ofisi ya misaada ya Imamu mkuu.

Biram Fall, Meneja Mkuu wa QNET Kanda ya Afrika chini ya jangwa la Sahara, wakati akitoa maoni kuhusu CSR ya Ramadhani ya QNET kwa mwaka huu, alisema:

"QNET imekuwa ikifanya hivi kwa miaka mingi. Kampeni ya kutoa msaada katika kipindi cha mwezi wa Ramadhan ni moja ya njia tunazotumia kuzifikia jamii kusaidia watu. Kadri tunavyoendelea katika biashara yetu, tunaamini katika kusambaza faraja na utoshelevu unaokuja pamoja nao. Kwa kweli ni muhimu sana, inatia moyo na inakamilisha jitihada za QNET. Inawezesha watu, inaonyesha upendo kwa jamii na pia inahamasisha wafanyakazi wetu na Wawakilishi wetu wa Kujitegemea (IRs), kadri wanavyoshiriki wao binafsi katika kuboresha maisha ya wengine. Malengo yetu ya kibiashara pia ni kuhusu kutengeneza fursa kwa watu, kufanya maisha ya watu kuwa bora na kuwawezesha watu kuwasaidia waweze kuishi maisha ya ukamilifu. Tunaita hiyo kuwa ni kuishi kikamilifu"

Mwaka jana, Kituo cha Uwajibikaji wa Mashirika kwa jamii cha Afrika ya Kusini kiliitunukia QNET kuwa kampuni bora ya mwaka ya kimtandao ya uwajibikaji kwa jamii (E-Commerce CSR Company of the Year) kwa uwajibikaji wake katika kusaidia jamii na kuleta mabadiliko bora.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: