Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz na viongozi wengine akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz na viongozi wengine akifunua pazia kuashiria kuzinduliwa kwa Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mikono wananchi kwa furaga huku akiwa na msichana baada ya kuzindua Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz alipowasili kuzindua Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz kuangalia Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo kabla ya kuvizindua huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi wa Ghala na Mitambo ya kuchakata Gesi ya LPG vya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz baada ya kuzindua Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz na na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Hamisi Ramadhani wakisiliza maelezo ya namna mitambo ya kuchakata gesi inavyofanya kazi wakati wa uzinduzi wa Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019. PICHA NA IKULU.

---
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 25 Juni, 2019 amezindua ghala na mitambo ya gesi ya mitungi inayotumika kupikia (Liquefied Petroleum Gas – LPG) inayomilikiwa na kampuni ya Watanzania iitwayo Taifa Gas Tanzania Limited katika Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Hamisi Ramadhani ameeleza kuwa uwekezaji mkubwa wa upanuzi wa ghala na mitambo ya gesi iliyopo Kigamboni umefanyika kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2018 ambapo umeongeza uwezo wake kutoka tani 1,650 hadi kufikia tani 7,650.

Uwekezaji huu umekwenda sambamba na ujenzi wa maghala na mitambo ya gesi katika Mikoa 20 hapa nchini kwa gharama ya shilingi Bilioni 150 na hivyo kuifanya Taifa Gas Tanzania Limited kuwa kampuni kubwa zaidi ya uwekezaji kwa idadi ya mitambo na kwa ukubwa wa ghala lenye mitambo ya kisasa kuliko yote Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Bw. Hamisi Ramadhani ameongeza kuwa uwekezaji huu umezalisha ajira za moja kwa moja 260 na zisizo za moja kwa moja 3,500 na kwamba pamoja na kuuza Tanzania kampuni hiyo inasambaza gesi katika nchini za Uganda, Rwanda, Burundi, DRC na Sudani Kusini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Azizi amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuweka na kusimamia mazingira yenye usawa kwa wafanyabiashara na wawekezaji wote na kwamba kutokana na mazingira mazuri ya kufanyia biashara anatarajia kuongeza uwekezaji wa miradi mingine yenye thamani ya shilingi Bilioni 500 katika miaka 3 ijayo.

“Msimamo wako thabiti dhidi ya matendo ya zamani ya ujanjaujanja katika biashara na uwekezaji, na ukwepaji wa kodi, ndivyo ambavyo leo hii vimetufanya baadhi yetu ambao kwa miaka tuliamua kuwekeza mitaji nje ya Tanzania, kupata moyo wa kuanza tena kurejesha mitaji hapa nyumbani” amesisitiza Bw. Rostam Azizi huku akitoa wito kwa wafanyabiashara wenzake kutambua kuwa milango ya uwekezaji Tanzania iko wazi kwa uwekezaji madhari wanafuata sheria, taratibu na kanuni za nchi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: