Mkurugenzi Msaidizi wa Uinuaji wa  Mazao, Pembejeo na Ushirika wa Wizara ya Kilimo Bw. Beatus Malema (kushoto) akizindua taasisi ya 'Wefarm' kwa kushika nembo jijini Dar es Salaam. Pembeni wakwanza kulia ni Meneja Mkuu wa taasisi ya 'Wefarm' Bw. Nicholus John na Mkuu wa Idara ya ufuatiliaji wa taasisi ya We Farm Bi. Cyrila Anton.


Mkurugenzi Msaidizi wa Uinuaji wa  Mazao, Pembejeo na Ushirika wa Wizara ya Kilimo Bw. Beatus Malema akizungumza wakati wa uzinduzi wa taasisi ya 'Wefarm' iliyofanyika leo 28 Juni 2019 jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa taasisi ya 'Wefarm' Bw. Nicholus John akizungumza na wakati wa uzinduzi wa taasisi hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi huo.
Mkuu wa Idara ya ufuatiliaji wa taasisi ya We Farm Bi. Cyrila Anton (picha ya juu) akitoa ufafanuzi zaidi masuala mbalimbali ya wakulima.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Taasisi ya 'WEFARM' imezinduliwa itakayowawezesha wakulima kubadilishana taarifa kwa njia za kidigitali.

Akizungumza na wanahabari wakati akizindua jukwaa la wakulima,Mkurugenzi Msaidizi wa Uinuaji wa  Mazao, Pembejeo na Ushirika wa Wizara ya Kilimo Bw. Beatus Malema

Amesema malengo ya serikali yetu nikuweza kufanya kazi pamoja na sekta binafsi, serikali za mitaa na watoa huduma wanaotoa huduma bora katika sekta ya Kilimo.

"Tunakaribisha Wefarm naninaimani kuwa mmekwenda kwa wahusika katika sekta ya kilimo na wamewasaidia kujua changamoto zinazo wakabili," amesema Bw. Beatus Malema.

"Jukwaa la Wefarm limetengenezwa kwa uwazi na litawawezesha wakulima toka pande zote za Tanzania kuweza kupata elimu, maarifa, kupashana habari na kutatua matatizo ili kuuza bidhaa zilizo bora." amesema Bw. Malema.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa WE FARM , Bw.Nicholaus John alisema huduma hiyo ni bure na mkulima atatuma ujumbe mfupi kupitia namba 15088.

“Mkulima ataweza kuuliza maswali na kupata majibu kutokana na matatizo mbalimbali yaliyopo shambani wkake, wazo hili lilikuja kutokana na kwamba wakulima wanachangamoto nyingin mashambani lakini wanakosa habari au ujuzi wa kuweza utatua matatizo yao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: