Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya anayetengeneza kundi la Wasafi Classic (WCB) Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinum akizungumza na wanahabari wakati akitangaza kuanza kwa Tamasha la Wasafi linalotarajia kufanyika hivi karibu katika mikoa mbali mbali nchini Tanzania.
Meneja wa Msanii Diamond Platinum Hamis Tale Tale a.k.a Babu Tale akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Wasafi litalotarajia kufanyika hivi karibuni.
Meneja wa Msanii Diamond Platinum, Said Fela akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Wasafi litalotarajia kufanyika hivi karibuni.
Mwakilishi wa BASATA, Prona Masenge akizungumza machache.
Mtaribu wa Masuala ya vijana TACAIDS, Grace Kessy akifafanua jambo.

Na Khadija Seif, Globu ya jamii.

MSANII wa muziki wa Kizazi Kipya anayetengeneza kundi la Wasafi Classic (WCB) Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinum amesema hakutegemea mapokezi ya kanyaga.

Diamond Platinum amesema mwaka huu umekua ni wa mafanikio makubwa kwake kutokana na nyimbo zake alizoziachia kupokelewa vizuri na mashabiki zake wa ndani na nje ya nchi.

"Mwanzoni mwa mwezi Mei niliachia "The one na badaae nikaamua nihamie kwenye midundo ya bolingo ambapo niliachia ngoma ya "INAMA" niliyomshirikisha Fally Ipupa kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na ilipokelewa vizuri sana na mwezi huu nimeachia "KANYAGA" ambayo pia imepokelewa vizuri sana na mashabiki,"

Aidha amesema ni baraka kupata Rais Dkt. John Pombe Magufuli anayejali, anaependa sanaa na hata hivyo ameendelea kuboresha kila sekta hasa kwenye upande wa usafirishaji ameleta ndege na amehakikisha kila mkoa kuna kuwa na viwanja vya ndege ili wasanii waweze kuwafikia mashabiki zao kwa wakati muafaka.

"Kuna vitu vingine Serikali ikivifanya watu wanavitafsiri vibaya na kuona kwa jicho la tofauti na ndiyo maana ndege zilivoletwa ilionekana Kama Serikali ya awamu ya tano inamaliza pesa kwenye kununua ndege lakini umuhimu wake unaonekana kwa sasa kutokana na usafiri unakua sio wa tabu tena,".

Diamond Platinum ametangaza rasmi kuwa Tamasha la Wasafi limezinduliwa rasmi na kwa mwaka huu litaanza kufanyika Julai 12 Muleba mkoa wa Kagera, Julai 14 mkoa wa Tabora huku ikifuatiwa na mkoa wa Iringa Julai 20 mwaka huu .

"Nina hamu sana na kufanya show Muleba kwani sijawahi kukutana na mashabiki zangu, hata hivyo sababu ya kuchagua mkoa wa Iringa ni kutokana na mapokezi yao mazuri kwa misimu iliyopita," amesema.

Pia amewataka mashabiki wategemee vitu vingi vizuri na vya tofauti kwa msimu huu wa nne wa tamasha la wasafi kuanzia jukwaa, mavazi, muziki na wasanii watakaotumbuiza.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: