Msanii wa Filamu Wema Sepetu akitoka katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo baada ya mahakama hiyo kutoa maamuzi ya kwenda Gereza la Segerea kwa siku nane. Wema aliingia matatani baada ya kutofika mahakamani hapo mara mbili hivyo mahakama ilitoa hati ya kumkamata kwa kuruka dhamana.
Msanii wa Filamu Wema Sepetu akiingia katika gari la magereza. 
Wema Sepetu akipaelekea kupanda gari la magereza baada ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa 
maamuzi ya kwenda Gereza la Segerea kwa siku nane. 

MAHAKAMA 
ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru msanii wa filamu Wema Sepetu kukaa  gerezani kwa siku nane wakati akisubiri maamuzi ya dhamana.

Wema aliingia matatani baada ya kutofika mahakamani hapo mara mbili hivyo mahakama ilitoa hati ya kumkamata kwa kuruka dhamana.

Akitoa maamuzi hayo leo, Hakimu Mkazi, Maira Kasonde alisema kutokana na  masuala yaliyoletwa mahakamani hapo yanahusu dhamana, atatoa uamuzi.

Alisema kesi hiyo itakuja Juni 24, mwaka huu hivyo mshitakiwa anatakiwa kukaa ndani hadi tarehe hiyo. 

Akijitetea kwanini asifutiwe dhamana, Wema alidai ni kweli hakufika mahakamani  Mei 11 na Juni 14, mwaka huu, ambapo alidai mara ya kwanza alisafiri  kikazi nje ya mkoa ambapo alikwenda mkoani Morogoro na kwamba alimpa  taarifa wakili wake.

Alidai mara ya pili, alifika mahakamani lakini alishindwa kuingia kwenye  chumba cha mahakama kusikiliza kesi yake kwa sababu aliumwa ghafla tumbo la hedhi.

Alidai  anapofika tarehe ya hedhi mara nyingi tumbo humuuma hivyo alienda  hospitali kwa ajili ya kuchomwa sindano ya diclopa. Hata hivyo, aliomba  mahakama imsamehe kwa kutokuhudhuria mahakamani.

Wakili wa Serikali, Glory Mwenda alidai mshitakiwa hana rekodi yakutohudhuria mahakamani hivyo mahakama impe onyo.

Pia alimtaka mshitakiwa endapo atapata udhuru kuwapa taarifa wadhamini wake ili kuepuka usumbufu kwa mahakama.

Juni 11, mwaka hu upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili Sylvia Mitanto  ulidai kwamba mshitakiwa hayuko mahakamani na hakuna taarifa yoyote.

Wema anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani.

Wema anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo  mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, ambapo alisambaza video za ngono  kupitia akaunti yake ya Instagram, picha ambazo inadaiwa kuwa haina  maudhui.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: