Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akizungumza na wananchi wa Njia Panda Chato wakati akielekea katika Kijiji cha Mlimani mara baada ya kuwasili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita kwa ziara binafsi ya siku mbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa Habari wa Mkoa wa Geita mara baada ya kuzungumza na wananchi waliofika katika uwanja wa ndege wa Chato.
Picha mbalimbali zikionesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita.
Picha mbalimbali zikionesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wakizungumza na wananchi waliofika katika uwanja wa ndege wa Chato.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa Habari wa Mkoa wa Geita mara baada ya kuzungumza na wananchi waliofika katika uwanja wa ndege wa Chato.

Na: Frank Shija – MAELEZO, Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kuwa Rais wa kwanza wa nje kutembelea Wilaya ya Chato.

Amesema kuwa ukiachilia mbali ujirani uliopo baina ya Tanzania na Kenya, pia kuna undugu kwa kuwa tunazungumza lugha moja, tunamuingiliano wa kijamii ikiwemo kuoana na kuwa na utamaduni unaofanana.

“Kufika kwako umeudhihirishia umma wa dunia kuwa sisi ni majirani, na marafiki wa kweli siku zote tutatembea pamoja kamwe tusikubali kulaghaiwa na watu,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema kuwa kutokana na ushirikiano huo wafanyabiasha wa Kenya na Tanzania wamekuwa wakishirikiana katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kijamii ikiwemo kuwekeza katika nchi zetu.

Kwa ujibu wa takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Kenya imewekeza miradi 504 yenye thamani ya dola 1.7 biloni ikiwa na idadi ya watu 50,956 huku wawekezaji wa Tanzania nchini Kenya wakiwa wakekezaji 24.

Aidha katika Sekta ya Utalii, Tanzania ni nchi ya pili kwa watu wake kutembela nchini Kenya ikitanguliwa na nchi ya Marekani ambapo kwa mujibu ya takwimu za Bodi ya utalii ya Kenya ya Mwaka 2018 Watanzania 222,216 walitembelea Kenya ambayo ni zaidi ya 10% ya watu wote waliotembelea Kenya.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli ameitaja miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kwa ushirikiano wan chi hizi mbili ikiwemo barabara ya Holili- Arusha hadi Namanga pamoja na maandalizi ya ujenzi wa Barabara kutoka Mombasa hadi Bagamoyo.

Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania ipo katika hatua mbalimbali za kujenga meli tano ambapo itaanzisha safari za kutoka Bukoba – Mwanza – Kisumu na Jinja.

Vile vile Rais Dkt. Magufuli ametoa wito kwa wawekezaji kutoka Kenya kuja kuwekeza nchini hapa kwa kuwa milango ipo wazi kwa mwekezaji yeyote na Watanzania waendelee kuwekeza Kenya ili kuendeleza ushirikiano uliopo kwa mustakabari wa maendeleo ya nchi zote mbili.

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyata amesema anayofuraha kuwa Rais wa kwanza wa nje kukanyaga ardhi ya Chato.

Ameongeza kwamba uwepo wake Chato Mkoani Geita ni udhibitisho kuwa nchi hizi ni ndugu na wapo kwa ajili ya kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Kenya.

“Hakuna mtu anayeweza kututenganisha kamwe, sisi kama watu wa Afrika Mashariki yatupasa kuhakikisha tunaondoa vikwazo vyote vitakavyozuia kutembeleana, kufanyabiashara pamoja na pengine hata kuoana.” Alisema Kenyatta.

Apongeza Ujenzi Uwanja wa Ndege Chato

Rais Kenyatta ameipongeza Serikali kwa kujenga uwanja wa ndege wa Chato kwa kuwa ni utaimarisha na kukuza ukuaji wa biashara na shughuli nyingine za kimaendelea katika ukanda huo jambo ambalo halipaswi kubezwa.

Amesema anashangazwa na baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakipuuza jitihada hizo za kujenga uwanja huo kwani ni muhimu na yeye kama Rais wa Kenya angependa kuona Afrika ya Mashariki inakuwa kitu kimoja.

Amechukizwa na kauli za baadhi ya wanasiasa na kusema haiwezekani kumzuia Mtanzania kufanya biashara au kuoa nchini Kenya vivyo hivyo kwa Wakenya nchini Tanzania.

Rais Keny
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: