Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa,mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.Rais Ramaphosa amewasili hapa nchini jana jioni kwa Ziara ya Kitaifa ya siku 3 na baada ya hapo atahudhuria Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwakaribisha wageni wao Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa na mkewe Dkt. Dk Tshepo Motsepe, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Rais Ramaphosa amewasili hapa nchini jana jioni kwa Ziara ya Kitaifa ya siku 3 na baada ya hapo atahudhuria Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa na mkewe Dkt. Tshepo Motsepe wakikabidhiwa maua ikiwa ni ishara ya upendo ya kuwakaribisha nchini,mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar na kupokewa na Rais Dkt John Pome Magufuli .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa wakati nyimbo za Mataifa hayo mawili zikipigwa katika hafla fupi ya mapokezi kwenye viunga vya Ikulu leo jijini Dar.
Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika viunga vya Ikulu, leo jijini Dar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakati nyimbo za mataifa mawili ya Tanzania na Afrika Kusini zikipigwa katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akikagua Gwaride la Heshma aliloandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakipunga mkono kwa wananchi wakati wakielekea kwenye mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuelekeza jambo Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimueleza jambo Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kabla ya kumpa zawadi ya Kinyago cha mpingo Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia zawadi ya picha aliopewa na mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. PICHA NA IKULU.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: