Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakisalimiana mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujumbe wa Wafanyabiashara toka Afrika kusini uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

Na Said Mwishehe, Michuzi TV.

RAIS Dk.John Magufuli wa Tanzania na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini wameeleza umuhimu wa uwekezaji katika miundombinu na kutumia fursa ya rasilimali zilizopo kukuza uchumi.

Marais hao wameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa kufungua Jukwaa la Biashara lililohusisha wafanyabishara, wawekezaji na maofisa wa serikali hizo.

Kwa upande wake Rais Cyril Ramaphosa, amesema kwamba uhusiano wa nchi yake na Tanzania ni wa muda mrefu na matarajio yao ni kuona ushirikiano unaendelezwa.

Amesema Afrika Kusini imaumia kwa tukio lililosababisha vifo vya watu zaidi ya 70 walioungua kwa moto.Hivyo anatoa pole kwa familia na majeruhi na kwamba wanamuomba Mungu awaponye.

Kuhusu mafanikio yao ambayo wamefikia nchini kwao leo hii amesema yanatokana na ushirikiano baina ya nchi zao na kwamba majadiliano ya Jukwaa hilo la Biashara yataonesha wapi waelekee kwa sasa.

"Tunapaswa kuwa na kauli moja ya wapi tunaelekea kibiashara ili kila nchi iweze kunufaika kwa maendeleo jumuisha," alisema.Alisema takwimu zinaonesha idadi ya watu itaongezeka siku zijazo hivyo ushirikiano huu unapaswa kuendelezwa kwa maslahi ya nchi zetu huku akieleza kuwa biashara itafanikiwa kama urasimu utaondolewa kwa kila pande.

Ametumia nafasi hiyo kueleza changamoto za kupata visa zinapaswa kuondolewa ili kuwavutia wafanyabishara na watalii.

Rais huyo wa Afrika Kusini amesema serikali yake imekuwa ikjadiliana na wafanyabishara kuhusu fursa zilizopo na kupata ufumbuzi.Pia amesema wanakaribisha kila mtu anayetaka kuwekeza kuingia kuwekeza ili kuchochea uchumi

Nchi zinatakiwa kuwekeza katika kukuza uchumi ili kusaidia huduma za jamii kwenye mitaa ambapo wawekezaji wanawekeza.Kwa upande wake Rais Magufuli amesema Tanzania imejipanga kuelekea uchumi wa viwanda ndio maana imeamua kuwekeza kwenye miundombinu kama kivutio cha wawekezaji kuja kuwekeza.

" Serikali imejipanga kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kuwekeza kwenye miundombinu naomba wawekezaji waje wawekeze na nyie nawaomba mjadala wenu ujikite kwenye mipango yetu sio mpeane namba halafu hakuna kinaendelea. Tunataka matokeo ya nyie kukutana yaweze kuwa na adhari chanya kwa nchi zetu kiuchumi, kijamii na maemdeleo, "amesema.

Alisema jukwaa hilo linaonesha dhamira nzuri ya nchi zetu kukuza uchumi, biashara na uwekezaji hivyo likitumika vizuri nchi zetu zitanufaika na kuongeza Afrika Kusini ni taifa kubwa ambapo bidhaa nyingi za Tanzania zimekuwa zikiienda Afrika Kusini hivyo kulifanya taifa hilo kuwa la pili kwa kununua bidhaa.

Pia amesema Tanzania inauza bidhaa nyingi Afrika Kusini ikiwemo madini hivyo na ni muhimu kuongeza uwekezaji wa viwanda kama vya usindikaji nyama, samaki na sukari.Rais Magufuli amewakaribisha wananchi wa Afrika Kusini kuja kuwekeza katika viwanda vya kuchenjua madini na vya dawa ili kupunguza gharama za kuagiza kutoka nje ya Bara la Afrika.

Amefafanua viwanda vya dawa vitaweza kusaidia kukuza uchumi wa nchi zetu .Wakati katika sekta ya utalii bado haijafanya vizuri na kuweza kusaidia maendeleo ya nchi."Tanzania ni ya pili duniani kwa vivutio vya utalii baada ya Brazili napenda kuwaomba wajumbe wa SADC mtembelee vivutio vyetu," alisema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: