RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein akifungua Mkutano wa kujadili utekelezaji wa bajeti na Mpango Kazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuanzia mwezi Julai 2018 hadi Juni 2019 na Uongozi wa Wizara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 21-8-2019. Kulia kwa Mhe. Rais ni Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma.
Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, kulia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma na Mshauri wa Rais Pemba Mhe Maua Abeid Daftari , wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, hayupo pichani akingoza mkutano huo wa Utekelezaji wa Bajeti na na Mpango Kazi wa Wizara hiyo, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
BAADHI ya Maofisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar , wakifuatilia Mkutano wa kupitia Utekelezaji wa bajeti na Mpango Kazi wa Wizara hiyo ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa bajeti na Mpango Kazi wa Wizara yake kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, wakati wa mkutano huo na Uongozi wa Wizara yake uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, 21-8-2019. 
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu ya Mafunzo ya Amali Zanzibar Dk. Idrisa Muslim Hijja akiwasilisha Utekelezaji wa bajeti na Mpango Kazi wa Wizara yake kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, Ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein. (Picha na Ikulu).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: