Serikali ya Mkoa wa Morogoro imetoa utaratibu kwa baadhi ya wadau wa maendeleo watakao penda kuchangia msaada wa vifaa tiba kwaajili ya majeruhi kupitia akauti ya bank ya NMB huku baadhi ya wadau hao wakiwemo shirika la hifadhi za Taifa Tanapa wakitoa msaada wa kiasi cha shilingi milioni kumi kwaajili ya wahanga wa ajali.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe akiwasikiliza kwa makini maofisa wa jeshi usu waliofika katika ofisi yake kwa mazungumuzo mbalimbali ikiwemo kutoa hundi ya shillingi milion 10 kwa ajiri ya kusaidia maafa yaliyotokea ya mkoani humo.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Kushoto mwenye koti jeusi Dkt. Kebwe Steven Kebwe akiongozana na maofisa wa jeshi usu mara baada ya kutoka kuona miili ya marehemu iliyokuwa nje ya chumba cha kuifadhia maiti .
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Steven Kebwe akipokea hundi ya shillingi millioni 10 kutoka kwa mhifadhi mkuu wa hifadhi milima ya udzungwa Donatus Dayona kwaniaba ya shirika la hifadhi za taifa TANAPA kwa lengo la kusaidia wahanga wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: