MKALI wa Muziki wa Kizazi Kipya ‘Bongo Fleva,’ ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwanga Kaskazini (ACT-Wazalendo), Manispaa ya Kigoma Ujiji, Clyaton Revocatus ‘Baba Levo,’ leo ameshinda rufaa yake katika Mahakama Kuu Kanda ya Magharibi (Kigoma).

Awali, Baba Levo alihukumiwa kifungo cha miezi 6 katika Mahakama ya Mwanzo Mwandiga, lakini alipokata rufaa Mahakama ya Mkoa, akahukumiwa kifungo cha Mwaka mmoja na siku mbili jela, kabla ya kukata rufaa upya, ambayo ameshinda leo katika Mahakama Kuu.

Diwani wa Kata ya Kigoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii, Hussein Kaliyango, amesema wanashukuru Mahakama Kuu kwa kutenda haki juu ya rufaa ya Baba Levo, ambaye alihukumiwa kwa kosa la kumshambulia Askari wa Usalama Barabarani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: