Mume wa Mtangazaji, Zamaradi Mketema, Shabani Hamisi leo Novemba 4, 2019 akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni na kusomewa shtaka la kumtishia kumuua kwa silaha aina ya Pisto, Venance John.
Mume wa Mtangazaji, Zamaradi Mketema, Shabani Hamisi leo Novemba 4, 2019 akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni baada ya kukizi masharti ya dhamana.

Na Karama Kenyunko.

MUME wa Mtangazaji, Zamaradi Mketema, Shabani Hamisi, leo Oktoba 4, 2019 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akikabiliwa na shtaka la kumtishia silaha aina ya Pisto, Venance John.

Hamisi amefikishwa mahakamani hapo kufuatia siku chache zilizopita kuonekana katika mitandao ya kijamii kupitia video iliyosambaa mitandaoni ikimuonyesha anamtishia silaha John ambaye ni dereva wa roli la Mchanga.

Akisoma hati ya mashtaka dhidi ya mshtakiwa huyo, wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Frank Moshi, kuwa Oktoba 30, 2019 maeneo ya Mbezi Mabwepande katika Wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Imedaiwa, siku hiyo, mshtakiwa Hamisi alikutwa na Pisto aina ya Beleta yenye namba ya usajili 102969 ambapo kwa makusudi alimtishia Venance John huku akijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria .

Hata hivyo, mshitakiwa amekana kutenda kosa hilo na ameachiwa huru kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya mahakama ambapo mahakama ilimtaka kuwa na wadhamini wawili wenye barua na vitambulisho vya Taifa ambapo walisaini Bondi ya Sh. Mil 2 kwa kila mmoja.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 13, 2019, mshitakiwa yupo nje kwa dhamana.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: