Mhe. Hassan Simba Yahaya Balozi wa Tanzania nchini Zambia, na Mhe. Mukela Manyindo Waziri Mkuu wa Jimbo la Mongu (katika ngazi ya kimila) wakikata utepe kuashiria mapokezi ya mbegu za korosho katika hafla iliyofanyika Mongu, Zambia.
Mhe. Hassan Simba Yahaya Balozi wa Tanzania nchini Zambia akihutubia adhira iliyojitokeza kwenye hafla fupi ya kukabidhi mbegu za korosho jimbo la Mongu, Zambia tarehe 16 Novemba, 2019

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi  shehena ya mbegu za korosho kwa Serikali ya Jamhuri ya  Zambia katika hafla iliyofanyika mjini Mongu nchini humo. 

Korosho hizo zimekabidhiwa kufuatia ahadi ya Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe  Magufuli aliyoitoa kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe.  Edgar Lungu kwenye uzinduzi wa Kituo cha Pamoja cha  Huduma Mpakani (OSBP) Tunduma tarehe Oktoba 5, 2019.

Katika tukio hilo Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Mhe.  Hassan Simba Yahaya Balozi wa Tanzania nchini Zambia, na kwa upande wa Zambia, Serikali aliwakilishwa na Waziri wa  Jimbo la Mongu Mhe. Richard Kapita, Watendaji kutoka Serikalini na viongozi wa Kimila.

Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Kapita kwa naiba ya Serikali ya Jamhuri ya Zambia ametoa shukurani za pekee kwa Mhe. Rais Magufuli kwa upendo aliouonesha kwa Zambia na kwa upekee kabisa kwa wananchi wa jimbo la Mongu.

Aliongezea kusema wananchi wa Mongu  wanamatumaini makubwa kuwa, mbegu hizo zitawapa 
chachu ya kuzalisha korosho kwa wingi na kunufaika kiuchumi kama ambavyo imekuwa kwa wananchi wa Tanzania
Mhe. Hassan Simba Yahaya Balozi wa Tanzania nchini Zambia (kushoto) na Waziri wa Jimbo la Mongu Mhe. Richard Kapita (kulia) wakijadili jambo muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhi na kupokea korosho iliyofanyika Mongu, Zambia 
Waziri wa Jimbo la Mongu, Zambia Mhe. Richard Kapita  akihutubia hadhira iliyojitokeza kwenye hafla ya  mapokezi ya mbegu za korosho
Mhe. Hassan Simba Yahaya Balozi wa Tanzania nchini Zambia, na Mhe. Mukela Manyindo Waziri Mkuu wa Jimbo la Mongu (katika ngazi ya kimila) wakikata utepe kuashiria mapokezi ya mbegu za korosho katika hafla iliyofanyika Mongu, Zambia 

Picha ya pamoja baada ya hafla ya kukabidhi mbegu za korosho
Mhe. Hassan Simba Yahaya Balozi wa Tanzania nchini Zambia (kushoto) na Afisa kutoka Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia wakifuatilia tukio lililokuwa likiendelea wakati wa hafla ya kukabidhi mbegu za korosho
Sehemu ya wananchi wa Mongu, Zambia waliojitokeza kwenye hafla ya mapokezi ya mbegu za korosho 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments: