Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (katikati) akinguzumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja kwa njia ya QR Code, wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliofanyika kwenye Tawi la Benki ya CRDB, Mlimani City jijini Dar es salaam, leo Machi 17, 2020. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Urio na kushoto ni Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Pwani, George Yatera.

Na Mwandishi Wetu.

Benki ya CRDB imezindua mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja
kwa njia ya QR Code.

Akizindua mpango huo Mkurugenzi wa Mawasiliano wa benki hiyo, Tully Esther Mwambapa alisema, Njia hiyo itamwezesha mteja kutoa maoni kwa Benki bila usumbufu wowote na kwa muda mfupi sana.

"Anachotakiwa kufanya mteja ni kuscan kwenye QR Code kwa kutumia simu yake ya smart ambayo imeunganishwa na internet, Mteja atafungua camera ya simu yake na kuscan kwenye QR Code ambazo zinapatikana kwenye matawi yote ya Benki halafu itampeleka moja kwa mojo kwenye website ya CRDB Bank, huko atakutana na maswali ambayo yatamwongoza kwenye kutoa maoni; ikiwa, kuona listi ya Matawi yote ya Banki ambayo atatakiwa kuchagua tawi ambalo anahitaji kulitolea maoni na baada ya hapo atatuma amoni yake, Maoni hayo yatakwenda moja kwa moja kwenye kitengo husika cha Benki ya CRDB na kufanyiwa kazi".

Aidha Mkurugenzi wa Mawasiliano amewataka wateja kutumia huduma hii kuwasilisha maoni yao amboyo kwanamna moja yatasaidia kuboresha huduma za kibenki na kuendelea kuwahudumia wateja wake kwa weledi mkubwa zaidi bila wasiwasi.

Uzinduzi wa mpango huo wa kutoa maoni, umeanza kutimiwa na Matawi matano ya jijini la Dar es salaam na baadaye  huduma hiyo itapatikana kwenye matawi na mawakala wote wa Benki hiyo
nchi nzima.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: