MAKAMANDA wa JWTZ wakiwa wamebeba jeneza la mwili wa Marehemu Ramadhani Haji Faki wakiingia katika viwanja vya Masjid Mushawar Muembeshauri Wilaya ya Mjini Unguja kwa ajili ya kuusala na kuuombea dua
NDUGU na Jamaa wa Marehemu Ramadhan Haji Faki Waziri Kiongozi Mstaaf wa Zanzibar, wakiwa wamebeba jeneza likiwa na mwili wa marehemu wakiingia katika Masjid Mushawar Muembeshauri Wilaya ya Mjini Unguja kwa ajili ya kumuombea marehemu.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akijuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika Sala ya kumuombea Marehemu Ramadhan Haji Faki Waziri Kiongozi na Bregedia Jeneral Mstaaf, ikiongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar. Sheikh. Saleh Omar Kabi, iliofanyika katika Masjid Mushawar Muembeshauri Wilaya ya Mjini Unguja, leo 29-3-2020.,
BAADHI ya Viongozi na Wananchi wakishiriki katika Ibada ya Sala ya Maiti kumuombea Marehemu Ramadhan Haji Faki, iliofanyika katika Masjid Mushawar Muembeshauri Wilaya ya Mjini Unguja leo,29-3-2020.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,.Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam wakiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika Sala ya kuuombea mwili wa Marehemu Ramadhan Haji Faki , iliofanyika katika Masjid Mushawar Muembeshauri Wilaya ya Mjini Unguja leo, 29-3-2020
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Kassim Majaliwa, wakisubiri kuwasili kwa mwili wa Marehemu Ramadhan Haji Faki, kijiji kwao Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa ajili ya hafla ya maziko hayo yaliofanyilka leo 29-3-2020.
BAADHI ya Wananchi wakihudhuria hafla ya maziko ya Waziri Kiongozi Mstaaf na Brigedia Jenerali Mstaaf Ramadhan Haji Faki yaliofanyika Kijiji kwao Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini Unguja leo.29-3-2020.
MAKAMANDA wa JWTZ wakiwa wamebeba jenela la mwili wa Marehemu Ramadha Haji Faki wakielekea katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya maziko katika Kijiji chao Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja yaliofanyika leo,29-3-2020.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein (kulia kwa Rais) Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na ( kushoto kwa Rais) Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar.Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo, wakiwa katika maziko ya Marehem,u Ramadhan Haji Faki, Waziri Kiongozi na Brigedia Jenerali Mstaaf, yaliofanyika Kijiji kwao Mkwajuni Mkoa wa Kaskaziuni Unguja leo.29-3-2020.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Ramadhan Haji Faki, wakati wa hafla hiyo ya maziko yaliofanyika katika Kijiji cha Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.
WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Ramadhan Haji Faki, wakati wa hafla hiyo ya maziko yaliofanyika katika Kijiji cha Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.
MKUU wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo, akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Ramadhan Haji Faki, wakati wa hafla hiyo ya maziko yaliofanyika katika Kijiji cha Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Kassim Majaliwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na Wananchi wakiitikia dua ikisomwa baada ya kumalizika kwa maziko ya Marehemu Ramadhani Haji Faki, yaliofanyika Kijiji cha Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 29-3-2020.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapiunduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein (kulia kwa Rais) Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe Kassim Majaliwa na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar. Brigedia Jenerali.Fadhil Omar Nondo, wakiwa wameshima wakati ikipingwa mizinga 17, wakati wa hafla ya maziko ya Brigedia Jenerali Mstaaf na Waziri Kingozi Marehemu Ramadhan Haji Faki yaliofanyika kijiji kwao Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 29-3-2020
ASKARI wa JWTZ wakitowa heshima wakati wa hafla ya maziko ya Marehemu Ramadhan Haji Faki Birigedia Jenerali Mstaaf yaliofanyika Kijiji kwao Mkoa wa Kaskazini Unguja.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akitowa wasifu wa Marehemu Waziri Kiongozi Mstaaf na Brigedia Jenerali Mstaaf. Ramadhan Haji Faki, yaliofanyika katika kijiji kwao Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.29-3-2020.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasalimia na kuwafariji Ndugu na Jamaa wa Marehemu Ramadhan Haji Faki, baada ya kumalizika kwa maziko yaliofanyika kijiji kwao Mkwajuni Mkoa wa Kaskaziniu Unguja leo 29-3-2020.(Picha na Ikulu)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein leo amongoza waombolezaji katika mazishi ya Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar, Brigedia Jenerali Mstaafu, Ramadhani Haji Faki yaliyofanyika Mkwajuni Zanzibar. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mazishi hayo, alipata fursa ya kutoa salamu za pole za Rais kwa wanafamilia na ndugu wa marehemu baada ya mazishi .

Akitoa salamu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Waziri wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Abood amemuelezea marehemu kuwa ni kiongozi aliyekuwa mstari wa mbele kutetea haki na kusimamia maendeleo katika nchi yetu.

“Aliweka mbele maslahi ya taifa na kuweka mbali maslahi yake binafisi ndiyo maana alishiriki katika vita kati ya Tanzania na Uganda vilivyomundoa madarakani Nduli Iddi Amini.”

Marehemu alizaliwa mwaka 1930 katika kijiji cha Mkwajuni, Kaskazini Unguja na mwaka 1983 hadi 1984 alikuwa ni Waziri Kiongozi wa Zanzibar.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu leo ametoa pole kwa familia ya Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine ambayo imeondokewa na Lazaro Edward Sokoine, aliyefariki Machi 28,2020 katika hospitali ya taifa Muhimbili alikokuwa akitibiwa.

Kwa mujibu wa msemaji wa familia Balozi Joseph Sokoine ambaye Pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, kesho kutakuwa na misa ya kumuombea marehemu kwenye kanisa katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro, Oysterbay jijini Dar es salaam. 

Amesema mazishi yanatarajiwa kufanyika katika kijiji cha Embwiki Monduli Juu keshokutwa
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: