Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli aakiongea baada ya kukikabidhi vitu mbalimbali kwa wawakilishi wa walezi na watoto wanaolelewa katika Kituo cha Nyumba ya Matumaini wakati wa hafla fupi ya kukabidhi misaada kwa vituo vya kulelea watoto wenye mahitaji iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Alhamisi Machi 19, 2020
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akikabidhi vitu mbalimbali kwa wawakilishi wa walezi na watoto wanaolelewa katika Kituo cha Cheshire Home wakati wa hafla fupi ya kukabidhi misaada kwa vituo vya kulelea watoto wenye mahitaji iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Alhamisi Machi 19, 2020.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akikabidhi vitu mbalimbali kwa wawakilishi wa walezi na watoto wanaolelewa katika Kituo cha Nyumba ya Matumaini wakati wa hafla fupi ya kukabidhi misaada kwa vituo vya kulelea watoto wenye mahitaji iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Alhamisi Machi 19, 2020.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli ametoa wito kwa taasisi mbalimbali, mashirika, wafanyabiashara na watu wenye mapenzi mema kujitolea kusaidia watu wenye uhitaji maalumu kwani kwa kufanya hivyo ni kutimiza amri kuu ya upendo ya Mwenyezi Mungu isemayo pendaneni kama mimi nilivyowapenda ninyi.

Mama magufuli ameyasema hayo wakati akitoa misaada mbalimbali kwa vituo vya kulelea watoto wenye mahitaji maalumu vya Cheshire Home na Nyumba ya Matumaini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Alhamisi Machi 19, 2020.

Mama Magufuli amekabidhi misaada hiyo kwa wawakilishi wachache wa watoto hao walioongozana na baadhi ya walezi wao, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa agizo la serikali la kuepuka mikusanyiko ya watu isiyo lazima kutokana na janga la ugonjwa wa mafua makali ya CORONA.

Mke wa Rais amesema hivi sasa ni kipindi cha Kwarezma ambapo ni kumbukumbu ya mateso ya Yesu Kristo, na kwamba kwa mujibu wa Isaya 58:7 waumini wanahimizwa kufunga, kuomba na pia kujitoa kwa wenzao wenye mahitaji mbalimbali.

“Kwa kuzingatia hilo nami leo nimewaita hapa ili kutoa kazawadi kangu kadogo kwa wanangu hawa”, alisema Mama Magufuli.

Misaada aliyotoa ni pamoja na mchele tani mbili, unga wa sembe tani mbili, maharage kilo 830, mafuta ya kupika lita 830, sukari, vinywaji, biskuti, sabuni za kufulia na kuogea, mafuta ya kupaka, mashuka, nguo, viatu pamoja na vyandarua.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: