Mtambo wa kisasa wa kuvunja mawe kwenye mfumo wa mkojo bila kutumia upasuaji ambao sasa upo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa na huduma hiyo itafanyika hapo kwa mara ya kwanza nchini.

Wataalam wa afya kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa wakifuatilia mkutano wa Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Dkt. Alphonce Chandika leo jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika akizungumza na wandishi wa habari hospitalini hapo jijini Dodoma akielezea upatikanaji wa huduma ya kuvunja mawe kwenye mfumo wa mkojo bila kufanya upasuaji. 

HOSPITALI ya Benjamin Mkapa ya jijini Dodoma imezindua huduma ya kwanza ya kisiasa ya kuvunja mawe kwenye mfumo wa mkojo bila kufanya upasuaji.
Huduma hiyo imezinduliwa baada ya kuwasili kwa mtambo wa kisasa unaotumia mionzi katika kufanya huduma hiyo tofauti na awali ambapo wagonjwa walikua wakifanyiwa upasuaji.

Akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dkt. Alphonce Chandika amesema huduma hiyo itafanyika kwa mara ya kwanza nchini na inawezekana ikawa ni mara ya kwanza pia kwa Nchi za Afrika Mashariki.

Dkt.Chandika amesema mtambo huo umekuja sehemu sahihi kwa sababu kanda ya kati yenye mikoa ya Dodoma na Singida imekua ikikabiliwa na changamoto ya wagonjwa wengi wenye matatizo ya mfumo wa mkojo.

"Tunashukuru sana serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli hakika tumejionea kwa vitendo utekelezaji wa ahadi zake haswa katika sekta ya afya. Mtambo huu unaenda kuwa mwarobaini wa tatizo la mfumo wa mkojo kwa wananchi wetu wengi.

Kanda ya kati imekua na idadi kubwa ya watu wenye changamoto hii. Kwa wiki tumekua tukipokea wagonjwa watatu hadi wanne wenye shida ya mfumo wa mkojo hasa mawe kwenye Figo, hivyo kuwasili kwa mtambo huu tuna uhakika kabisa unakwenda kuwa msaada kwetu na kwa wagonjwa," Amesema Dkt. Chandika.

Aidha Dkt. Chandika pia amesema Hospitali ya Benjamin Mkapa pia imechukua tahadhari ya kupambana na maambuziki ya virusi vya Corona kwa kuweka utaratibu wa kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na yenye 'sanitizer' kwa kila mtu anaeingia na kutoka hospitalini hapo.

" Katika kuchukua tahadhari pia tumetoa tangazo kwa wagonjwa na wananchi wetu kuwa idadi ya ndugu watakaokuja kuwaona wagonjwa haitozidi wawili ili kuepuka msongamano usio wa lazima, lakini pia tumeweka sanitizer na maji kwa ajili ya kujikinga na maambukizi," Amesema Dkt. Chandika. 

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: