Wakuu wa Mikoa ya Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka, Morogogo – Mhe. Loata Sanare, Tanga – Mhe. Martine Shigela na Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakiweka shada la maua katika kaburi la Alazaro Sokoine, Monduli Mkoani Arusha

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo ameongoza watumishi wa Ofisi yake katika mazishi ya Alazaro Sokoine ambaye ni mtoto Mkubwa wa Hayati Edward Moringe Sokoine. Mazishi hayo yamefanyika jana Monduli Juu Mkoani Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, ndugu, jamaa na Marafiki.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine (kushoto) akiweka shada la maua pamoja wanafamilia katika kaburi la kaka yake mkubwa Alazaro Sokoine. Mazishi yamefanyika jana Monduli Mkoani Arusha.
Mkurugenzi wa Utawala na usimamizi wa Rasilimali watu Bi. Emma Lyimo akitoa heshima za mwisho katika ibaada ya kuaga mwili wa Alazaro Sokoine ambae ni mtoto mkubwa wa Hayati Edward Moringe Sokoine. Mazishi yamefanyika jana Monduli Mkoani Arusha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: