Mlipuko wa homa kali ya mapafu, COVID-19 au Virusi vya Corona, umeleta athari katika nyanja mbalimbali za kiuchumi kote duniani, ikiwemo sekta ya ajira. 


Baadhi ya makampuni yamelazimika kupunguza idadi ya waajiriwa, mengine yakilazimika kufunga biashara na uzalishaji, huku mengine yakisaidia juhudi za seriali na hata sekta binafsi kukabiliana na matokeo ya mlipuko wa virusi vya Corona ili kusaidia kurudisha mataifa katika hali ya kawaida ya uzalishaji. 

Hapa Tanzania, makampuni Mengi yamechangia rasilimali katika juhudi za serikali na za taasisi za tiba kwenye kukabiliana na maradhi hayo. 

Vile vile, makampuni mengi ya ajira, ikiwemoBrighterMonday Tanzania, kampuni kubwa zaidi inayojihusisha na ajira na rasilimali watu, imechukua hatua kuangazia changamoto za udhibiti rasilimali watu pamoja na changamoto zinazowakabili waajiri
nchini Tanzania. 

Katika utafiti wao, BrighterMonday imewahoji maafisa rasilimali watu kutoka sekta mbalimbali za ajira nchini na kuwauliza changamoto wanazokutananazo katika kuajiri hasa wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona. 

Maofisa hao wameeleza kuwa wanapitia wakati mgumu kupata watu wenye vigezo vinavyohitajika kwa ajili ya kuwaajiri bila kuonana nao ana kwa ana kwa ajili ya usaili.

 Changamoto hii ndiyo iliyofanya kampuni ya BrighterMonday kubuni njia mbadala ya kusuluhisha tatizo hilo. 

Akizungumzia hili, Mkurugenzi wa BrighterMonday Tanzania, Reshma Bharmal-Sharriff amesema kuwa wanaelewa changamoto zinazowakabili kibiashara na chagamoto za maafisa rasilimali watu nchini. 

"Kwa kulitambua hili, tunatoa ofa ya matangazo ya kazi kwa wateja wetu wote kwa muda wa miezi mitatu kuanzia mwezi huu wa Aprili hadi June ili kuhakikisha kuwa waajiri wanafanya kazi zao katika mazingira mazuri," amesema Reshma.

Ameongeza kuwa kampuni yake imejipanga kujitoa kuwasaidia wale wote walio katika mstari wa mbele kupambana na maambukizi ya virusi vya corona kwa kutoa punguzo kwa baadhi ya huduma za ajira. 

"Lengo letu ni kuhakikisha kuwa waajiri wanakuwa na watu sahihi wanaowahitaji kwa ajili ya kazi zao." 

Reshma ameongeza kuwa kampuni yake inahakikisha kuwa wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona mchakato wa kuajiri unakuwa mzuri na wenye faida.

 "Kwa kutumia mfumo wa Uainishaji wa Ujuzi wa BrighterMonday, tunataka kuhakikisha kuwa waajiri wanaridhika na mfumo wa usahili na waajiriwa watakaopatikana watakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya kazi kama walivyoainisha katika vyeti vyao, amesema Reshma. 

Bi. Reshma anaeleza kuwa kampuni yao imeandaa mfumo wa uchakataji wa taarifa za mwombaji ambao unaweza kumsaidia mwajiri kuchambua sifa kadhaa za mwombaji, ikiwemo kiwango cha elimu na ujuzi alionao. 

Hii inamwezesha mwajiri kuweza kulinganisha kwa urahisi vigezo anavyohitaji ili kumpata mtu sahihi atakayemwajiri kwa muda mfupi na kwa umahiri mkubwa. 

Kampuni hiyo imejipanga kuwasaidia waajiri kuchambua na kupata waombaji watakaofaa kwa kazi wanazohitaji bila kujali hali ya kiuchumi inayoikabili dunia kwa sasa. 

Hivyo, kama unahitaji kupata wafanyakazi bora wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona, unaweza kufanya hivyo kwa 
urahisi.


Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: