Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam imemuhukumu Mkurugenzi wa Jamii Forums, Bw. Maxence Mello kulipa faini ya Shilingi Milioni 3 ama kwenda jela mwaka mmoja baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuzuia Polisi kutekeleza majukumu yao.

Aidha mahakama hiyo imemuachia huru mshtakiwa mwenzake Bw. Mike Mushi baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha wa kumuhusisha na kosa. Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Bw.Thomas Simba ndiye aliyetoa hukumu hiyo. Pichani chini Bw.Mello na mwenzake Mushi wakiwa kwenye mahakama hiyo leo Aprili 8, 2020 wakati na kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo.

Aidha Bw. Maxence Mello ameweza kulipa faini hiyo na kuachiwa huru.
Mkurugezi mtendaji wa mtandao wa kijamii wa Jamii Forums Maxence Mello (kushoto) na mwenzake,m Mike Mushi (katikati) wakiwa na wakili wao, Jebra Kambole wakitoka mahakama ya Kisutu Aprili 8, 2020 baada ya kulipa faini ya shilingi milioni tatu na hivyo kukwepa kifungo cha mwezi mmoja jela.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: