Na Winfrida Mtoi.

SIMBA inafanya mawindo yake kimya kimya kama ilivyofanya katika usajili wa msimu huu ambao wachezaji wengi waliowasajili ilikuwa ‘surprise’ kwa wadau wa soka nchini.

Licha ya Wekundu wa Msimbazi hao kutoweka wazi kuwa wameanza harakati za kuboresha kikosi chao, DIMBA Jumatano linafahamu tayari kuna nyota ambao majina yao tayari yako mezani.

Katika tetesi za usajili kwa sasa wakati ambao Ligi Kuu Tanzania Bara inaelekea ukingoni, wapo nyota kadhaa wanahusishwa kutua Msimbazi.

Simba ambayo ina uhakika wa kutetea ubingwa wake na kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, inataka kuongeza nguvu katika maeneo yaliyoorodheshwa katika ripoti ya kocha mkuu, Sven Vandenbroeck.

Kati ya sehemu ambazo zinatajwa zaidi na kuhitaji watu ni safu la ulinzi na ushambuliaji. Majina ya nyota ambayo DIMBA imepenyezewa kutoka ndani ya Simba ni kama ifuatavyo;

Baraka Majogoro: Ni kiungo anayefanya vizuri na timu ya Polisi Tanzania, alisajiliwa msimu huu na klabu hiyo akitokea Ndanda FC na mkataba wake na maafande hao unafikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu.

Bakari Mwamnyeto: Inasemekana tayari alishasaini mkataba wa awali wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo ya Msimbazi akitokea Coastal Union.

Beki huyo wa kati aliyezivutia timu nyingi baada ya kuonesha kiwango kizuri katika kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars, katika mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Afrika kwa wachezaji wa ndani maarufu CHAN, aliposimama na Erasto Nyoni.

Idd Mobby: Kifaa kingine cha Taifa Stars na Polisi Tanzania, anacheza safu ya beki wa kati, msimu uliopita alichezea Mwadui FC ya Shinyanga.

Sogne Yacouba: Ni straika wa Asante Kotoko ya Ghana, raia wa Bukinafaso, inadaiwa kuwa Simba wanawinda saini yake na mkataba wake unatarajia kumalizika mwezi huu.

Yacouba mwenye umri wa miaka 28, anafukuziwa na timu nyingine ikiwamo Azam FC, Lamontville Golden Arrows, Free State Stars za Afrika Kusini na Legon Cites inayoshiriki Ligi Kuu Ghana

Hassan Kibailo: Ni beki wa kulia wa Coastal Union, naye anahusishwa kutua Msimbazi ili kumuongezea nguvu Shomari Kapombe.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: