Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisoma maelezo baada ya kuzindua Muongozo wa Mpango wa Watoa huduma ya Afya ya Jamii, Dar es Salaam jana. Wizara ya Afya imezindua muongozo huwa ikiwa ni muendelezo wa kuendelea kutoa kipaumbele katika kuimarisha huduma za kinga, ikiwemo elimu ya afya na uhamasishaji, lishe, udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza kama Ukimwi na afya ya mama na mtoto.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Ummy akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Muongozo wa Mpango wa Watoa huduma ya Afya ya Jamii, Dar es Salaam jana. Wizara ya Afya imezindua muongozo huwa ikiwa ni muendelezo wa kuendelea kutoa kipaumbele katika kuimarisha huduma za kinga, ikiwemo elimu ya afya na uhamasishaji, lishe, udhibiti
wa magonjwa ya kuambukiza kama Ukimwi na afya ya mama na mtoto. 


Serikali ya awamu ya Tano imesema kuwa itaendelea kutoa kipaumbele katika kuimarisha huduma za kinga, ikiwemo elimu ya afya na uhamasishaji, lishe, udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza kama Ukimwi na
afya ya mama na mtoto.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika
uzinduzi wa muongozo wa mpango wa huduma za afya katika jamii na
matumizi ya dashibodi ya viashiria vya elimu ya afya kwa umma jijini Dar
es Salaam leo.

“Hii itasaidia juhudi za kupunguza mzigo wa
gharama za matibabu unaowatesa wananchi na kuongeza matumizi ya serikali
katika tiba ya magonjwa yanayoweza kuzuilika au kuepukwa,” alisema
waziri.

Alisisitiza kuwa umuhimu wa huduma za kinga ambao
umezingatiwa katika Sera ya Taifa ya Afya ya mwaka 2007 na Mpango
Mkakati wa Sekta ya Afya wa Mwaka 2015 – 2020 utakuwa kipaumbele katika
maandalizi ya Sera Mpya ya Afya ya Mwaka 2020.

Mkakati huu wa
kutumia watoa huduma za afya kwa jamii utawezesha kuwepo kwa huduma
imara za kinga katika ngazi zote ikiwemo utoaji elimu ya afya na
uhamasishaji kama njia muhimu ya kusaidia jamii zetu kujikinga na
magonjwa.

Serikali inatambua kuwa jamii yenye elimu sahihi juu
ya vyanzo vya afya bora na masuala yanayoweza kuathiri afya hufanya
maamuzi sahihi juu ya mambo yanayohusu afya zao.

Hii
itawezesha Taifa letu kuwa na wananchi wenye afya njema wanaochangia
katika maendeleo yao, familia zao, jamii wanayoishi na nchi yetu kwa
ujumla.

Amesema kuwa serikali imeendelea kuimarisha huduma za
afya ili kufikia malengo ya upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi
wote yaani Universal Health Coverage ambavyo itajumuisha utoaji elimu ya
afya juu ya mambo yahusuyo lishe, afya ya uzazi, watoto na vijana
ikijumuisha magonjwa ya mlipuko kama COVID-19 pamoja na magonjwa
yasiyoambukiza.

Pia jitihada hizi zinalenga kuhamasisha
matumizi ya bima za afya ili kuwawezesha wananchi kutumia huduma
mbalimbali za afya wanapohitaji.

Kwa mfano katika kipindi cha
miaka mitatu iliyopita tumeshuhudia ongezeko la idadi ya watu
waliopatiwa huduma za magonjwa yasiyoambukizakutoka watu milioni 3.4
(3,386,067) mwaka 2016 hadi wagonjwa Milioni 4.2 (4,190,467) mwaka 2018
ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 24 ya wagonjwa hao.

Sambamba
na takwimu za wagonjwa, pia tumeshuhudia ongezeko la vifo vitokanavyo
na magonjwa yasiyoambukiza hadi kufikia asilimia 33 ya vifo vyote nchini
kwa mwaka 2017, ambapo jumla ya vifo 134,600 viliripotiwa na kuhusishwa
na magonjwa yasiyoambukiza.

Huku vifo vitokanavyo na magonjwa
ya moyo na shinikizo la damu vikichangia kwa asilimia 13, idadi ambayo
ni kubwa kuliko ile itokanayo na magonjwa kama Ukimwi, Kifua Kikuu au
Malaria.

Waziri Mwalimu alisema kuwa matatizo yote haya
yanaweza kupunguzwa kwa kiasi kikubwa sana endapo tutaimarisha mifumo ya
kutoa elimu na taarifa sahihi kwa jamii zetu juu ya namna ya kuepuka
kwa kufuata kanuni bora za afya pamoja na kuwatumia vyema wahudumu afya
za jamii kuanzia ngazi za kijiji na mtaa.

Na hayo yote sasa
serikali inataka yakafanywe na wahudumu wa afya wa jamii ambao baada ya
tathmini mpya kufanyika wataongezwa kwa baadhi ya vijiji ambavyo ni
vikubwa na pia watapatiwa mafunzo maalumu namna ya kukabiliana kutoa
elimu sahihi kwa wananchi kuhusu magonjwa Haya.

“Pia Wahudumu wa
afya ya jamii hawa waende wakahamashishe jamii zetu kujenga desturi ya
kutafuta huduma rasmi za afya ikiwa ni pamoja na kujiunga kwenye mifuko
yetu ya bima za afya ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya,”
alisisitiza.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Miradi ya USAID
Tulonge Afya Bw Waziri Nyoni ameipongeza serikali kwa maamuzi ya
kuufanya mfumo huu wa wahudumu wa afya wa jamii kwa kuufanya uwe rasmi
tofauti na awali ambapo kila mdau alikuwa akitumia mfumo wake hivyo kuwa
na changamoto nyingi.

Alisema kuwa USAID Tulonge Afya imekuwa
ikitumia mfumo wa wahudumu wa afya ya jamii kufanikisha miradi yake
mingi ya afya hapa nchini.

Kwa mfano hadi sasa kuna takribani
watoa huduma wa afya ya jamii 2200 waliopo katika mikoa 12 na wilaya 29
huku wakitoa baadhi ya huduma wanazozitoa ikiwa ni pamoja na
uhamasishaji masuala ya Afya kama malaria, Afya ya mama na mtoto,
ukimwi, kifua kijua, na mengine mengi.

Naye Mkurugenzi wa
Utafiti, tathmini na Ufuatiliaji, FHI360, Dr Joseph Msofe alisema kuwa
kupitia mradi wa USAID Tulonge Afya, wameshirikiana na wizara kuandaa
mfumo wa upokeaji na utoaji wa taarifa ambao umeunganishwa katika mfumo
rasmi wa Wizara yaani DHIS2.

Kutokana na hili, watoa huduma za
afya ngazi ya Jamii au mdau yoyote atakua anafanya shughuli za
uhamasishaji jamii ina maana atatakiwa kufuata mfumo na utaratibi huu
mzuri na taarifa zote zitaonekana katika ngazi ya wilaya hadi taifa na
hivyo kuwawezesha watendaji na watoa maamuzi kujua ni nani anafanya nini
na wapi na hivyo kusaidia katika kufanya maamuzi sahihi..


Lakini pia mfumo huu wa ufuatiliaji na utoaji taarifa utasaidia
watendaji ngazi zote katika masuala ya afya kuufanya ufuatiliaji ili
kubaini penye mapungufu hivyo kuongeza kufahamu maeneo ambayo ufanisi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: