Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo katika Ukumbi wa wizara, jijini Dodoma, ambapo ameahidi kuwashughulikia watendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) wasiotoa huduma stahiki kwa wananchi wanaofika kuomba vitambulisho.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dkt. Anold Kihaule (kulia) wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo katika Ukumbi wa wizara, jijini Dodoma, ambapo ameahidi kuwashughulikia watendaji wasiotoa huduma stahiki kwa wananchi wanaofika kuomba vitambulisho
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akijibu maswali ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika leo katika Ukumbi wa wizara, jijini Dodoma, ambapo ameahidi kuwashughulikia watendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) wasiotoa huduma stahiki kwa wananchi wanaofika kuomba vitambulisho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Serikali imesema mashine chakavu ndio chanzo cha ucheleweshaji wa vitambulisho vya NIDA kwa wananchi wake hapa nchini, na badala yake wamenunua mashine mpya yenye thamani ya sh bilion 8.5 yenye uwezo wa kufyatua vitambulisho 9000 kwa saa. 

Mpaka sasa tayari NIDA imefanikiwa kutoa vitambulisho milioni sita na kutambua wananchi milioni 21. 8, hadi sasa kati ya watu 27. 7 waliotarajiwa kusajiliwa. Jumla ya namba za kipekee za utambulisho ni milioni 17. 8 zilikiwa zimezalishwa na zinaweza kutumika katika utambuzi wa watu. 

Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene alisema tayari serikali imenunua mashine mpya ambazo zitakamilishwa kufungwa April mwaka huu kwa ajili ya kuanza kufanya kazi. 

Alisema mtambo huo mpya una uwezo wa kuzalisha vitambulisho 9, 000 kwa saa jambo ambalo kwa siku nzima wanauwezo wa kutoa vitambulisho vya kutosha kwa wananchi wake. 

Alisema mitambo mipya na ikishirikiana na ile ya zamani wanaamini watatoa vitambulisho vingi ambapo wanatarajia kukamikisha zoezi hilo ndani ya miaka miwili. “Safarii hii vitambulisho vitakuwa bora awali vilivyotolewa havikuwa na ubora kutokana na mashine kuwa chakavu, ” alisema Simbachawene. 

Alisema awali mtambo ulikiwa ukizalisha vitambulisho 500 lakini hivi sass vitaboreshwa na kuzalishwa vitambulisho vingi kwa siku ili kukamilisha zoezi hilo. Hata hivyo aliwaomba radhi wananchi kutokana na kupata shida katika zoezi hilo hivyo amewaahidi hivi sasa litafanyika kwa haraka zaidi. 

Alisema mashine hizo ni bora na zitafanikiwa kukamikisha zoezi hilo ndani ya miaka miwili kwa watanzania wote au pungufu ya miaka hiyo. Alisema serikali ilivyojipanga kutekeleza zoezi hilo mamlaka imeendelea na ukamilishaji wa ufungaji mashine wa mitambo ya kisasa yenye uwezo mkubwa wa kuzalisha vitambulisho 9, 000 kwa saa moja na zoezi la uzalishaji vitambulisho litaanza mwishoni mwa Aprili. 

Nida kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji Kamati za Ulinzi na usalama Idara ya wakimbizi na Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA. Waziri Simbachawene alisema kutokana na utendaji usioridhisha wanatarajia kufanya mabadiliko ndani ya NIDA ili kuboresha. 

Alisema pia watakuwa makini katika ugawaji wa vitambulisho kwa wageni wakaazi na wakimbizi. Zoezi la utoaji vitambulisho litaendelea ambapo hadi sasa ni watu milioni sita pekee ndio wamekabidhiwa vitambulisho vya taifa kati ya milioni 27. 7 waliotarajiwa kusajiliwa
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: