Mratibu wa Kamati ya Programu ya mapambano dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona kutoka TYEC Mkoa wa Singida, Stella Mwagowa (kulia) akitoa elimu ya namna ya kujikinga na Virusi vya Corona kwa Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja na wafanyakazi wa mabasi katika stendi kuu ya mabasi mkoani hapa. 
Macmillan Marco, kutoka TYEC akitoa elimu hiyo kwa abiria ndani ya basi. 
Mmoja wa Wanajumuiya ya TYEC, Richard Assey, akionesha namna ya kujipaka Sanitizer kwa ajili ya kujikinga na Virusi vya Corona.
Baadhi ya Vijana kutoka TYEC wanaojitolea kutoa elimu ya mapambano dhidi ya kuenea kwa ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na Virusi vya Corona wakitoa elimu hiyo kwa wafanyabiashara walio na vibanda vyao kuzunguka Stendi ya Mabasi mkoani hapa.
Mratibu wa Kamati ya Programu ya mapambano dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona kutoka TYEC Mkoa wa Singida, Stella Mwagowa, akionesha jinsi ya kunawa ili kujikinga na Virusi vya Corona.
Afisa wa Polisi, Rashid Mirambo, akitoa elimu ya namna ya kujikinga na Virusi vya Corona kwa . Kushoto ni Mwenyekiti wa TYEC, Mkoa wa Singida, Stanley Roman.
Macmillan Marco (kulia) kutoka TYEC akitoa elimu hiyo kwa wafanyabiashara waliopo stendi ya mabasi mkoani hapa.
Elimu ya kujikinga na Virusi vya Corona ikiendelea kutolewa.
TYEC wakijadiliana baada ya kutoa elimu hiyo stendi ya mabasi mkoani hapa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: