Jiulize kabla ya kuja wazungu wazee wetu walikua wakijitibu vipi? Ushahidi wa kihistoria unaonesha wazee wetu walikua wakifanya hata aina mbalimbali za upasuaji.

Wakoloni walipokuja wakawa wanabeza kila kitu chetu ili kutengeneza hali ya kujidharau na kuwatukuza wao (inferiority).

Walitufanya tuone dawa zetu ni ushirikina huku wakizichukua kwa usiri na kwenda kutengeneza dawa za kisasa. Waliosoma pharmacology wanaelewa hili.

Kule kwetu Upareni, walichukua mti wa mkwinini na kutengeneza dawa ya vidonge vya Quinones ambavyo WaAfrika tulirudi kuuziwa kwa gharama kubwa.

Kuhusu magonjwa ya mafua na kifua dawa za asili zimeonesha ufanisi mkubwa sana. Nenda kwenye duka la dawa zinazoitwa za kisasa halafu uliza dawa ya kifua kutoka India, utakuta kichupa kimeandikwa alternative medicine.

Ni hapahapa Tanzania ambapo wazungu walikuja miaka ya 2010 na kuchukua magome ya mjaafari kisha kutengeneza dawa ya kutibu kifua ambazo tulizinunua shilingi 40,000 kwa kichupa kimoja.

Tuko tayari kununua kwa gharama kubwa dawa za asili zitokazo nje kwa gharama kubwa kuliko kutumia zinazopatikana katika mazingira yetu. Enyi WaAfrika ni nani aliyewaroga?

Viongozi wa Afrika waliweka siku maalumu katika kila mwaka ya kuadhimisha dawa za asili ili tufahamu umuhimu wake. Wakati mwengine watu hufa kwa laana ya kudharau cha kwao.

Wizara ya Afya nayo ikaanzisha Baraza la Dawa za Asili kwasababu inafahamu umuhimu wa dawa hizo.

Tuendelee kumpuuza Rais tukingojea dawa itafitiwe Ulaya tuletewe? ndio maana WaAfrika tumegeuzwa panya wa maabara kutokana na ujinga na utumwa wa akili tulionao.

Kujifukiza kupo mpaka ulaya ambapo wanaita inhalation miti ya kizungu kama anise na licorice imekua ikitumika tangu zama za Socrates.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: