Mkuu wa Wilayani ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa akifungua semina ya wafanyabiashara wa badari ya Bagamoyo iliyofanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo mkoa Pwani.
Mtafiti Mwandamizi wa Teknolojia ya Nyuklia, Alex Pius Muhulo akizungumza na wafanyabiashara wa badari ya Bagamoyo wakati wa semina ya utambuzi wa vifaa vyenye miozi iliyofanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Sehemu ya wafanyabiashara wa badari ya Bagamoyo wakisikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa (hayupo pichani) alipo kuwa akifungua semina ya utambuzi wa vifaa vyenye mionzi.
Mkuu wa Wialaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa (kulia) akiteta jambo na wafanyabiashara wa bandari ya Bagamoyo baada ya kufungua semina wilayani humo.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mkuu wa Wialaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara. 

WAFANYABIASHARA wadogo wa bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani, wamepata elimu ya utambuzi wa bidhaa na viaa vyenye mionzi ikiwa ni hatua za kuwaelimisha ili wajitambue na wajue jinsi ya kujikinga.

Hayo yamebainishwa leo mjini Bagamoyo kwenye semina ya siku moja ya mafunzo hayo kwa wafanyabiasara wadogo wa naotumia bandari hiyo na Kaimu Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Alex Muhulo.

Alisema TAEC imerahisisha huduma kwa wafanyabiashara wadogo wanaoingiza bidhaa nchini, kwa kufungua ofisi katika maeneo ya mipakani na bandarini na kupima sampuli za bidhaa husika kisha kutoa majibu ndani ya muda mfupi hivyo kuokoa muda wa mfanyabiasha huyo.

Akizungumzia maboresho ya utendajikazi wa TAEC na mfumo wa utoaji huduma kwa njia ya mtandao hususan kwa wafanyabiashara wadogo, Muhulo alisema hadi sasa tume hiyo imeshafungua ofisi 24 kwenye mipaka mbalimbali nchini ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa kundi la wafanyabiashara hao wasio na uwezo wa kufuata huduma hiyo kwenye ofisi za Kanda au makao makuu.

Alex amewataka wafanyabiashara hao kutambua kwamba bidhaa zina mionzi hivyo ni vyema wakafuata taratibu za kisheria za uingizaji wake kutoka nje ili ziwe salama na zisilete madhara kwao na kwa watumiaji wa mwisho.

Kuhusu kuboresha mfumo wa utoaji huduma za TAEC mtandaoni, Muhulo alisema tume hiyo imejipanga kuhakikisha wafanyabiashara wanapata huduma kwa muda mfupi ili kusiwe na kikwazo cha utoaji bidhaa zao bandarini na kusababisha hasara.

Kwa sasa wafanyabiashara wadogowadogo wanaoingiza bidhaa zao nchini kupitia bandari mbalimbali wanapata huduma bandarini hapo na pia sampuli huchukuliwa na majibu kurudishwa muda mpufi ya kutambua kiwango cha mionzi kilichopo ikiwa hatua ya udhibiti wa uingizaji wa bidhaa hatari kwa binadamu, viumbe hai wengine na mazingira.

Aidha , Alex aliongeza mafunzo mengi kama hayo yameshatolewa kwenye maeneo mbalimbali ya jinsi ya kudhibiti uingizaji wa mionzi hatarishi na kwamba kwa sasa hali ya mionzi nchini ni nzuri na inadhibitiwa vizuri kuhakikisha nchi iko salama.

Mafunzo hayo yalifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa ambaye alisema mafunzo hayo yatawasaidia wafanyabiashara hao kuwa na elimu ya mionzi na kutambua jinsi ya kujikinga.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: