Kada wa chama chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa vijijini Adestino Mwilinge ajitosa kugombea jimbo la Isimani

NA FREDY MGUNDA, IRINGA.

MBUNGE wa jimbo la Isimani William lukuvu amenza kuupata upinzani ndani chama cha mapinduzi (CCM) mara baada ya kada wa chama hicho Adestino Mwilinge kutangaza kutia nia ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge wa jimbo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika kijiji cha Mbuyuni kada huyo alisema kuwa ameamua kutia nia kwa mijubu wa kanuni na katiba ya chama hicho inavyosema kila mwananchama anahaki ya kuchaguliwa na kuchagua kwa mujibu wa ibara ya 14 (3) na 15 (1).

Alisema kuwa ameamua kutia nia akiwa kijijini kwao kwa lengo la wadau watambue kuwa yeye ni mkazi wa jimbo la Isimani na anania ya dhati ya kusaidia kuleta maendeleo kwa wananchi wanaishi katika jimbo hilo.

Mwilinge alisema ameamua kutia nia baada ya katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Dr Bashir Ally Kakurwa kutangaza wanachama wa chama hicho wanaruhusiwa kutia nia kwa kuwa ni wajibu wao kulingana na katiba ya chama hicho.

Aliongeza kuwa anaunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuleta maendeleo ya nchi hii katika kipindi hiki cha miaka mitano aliyokuwa madarakani.

Kada huyo aliyehudumu katika chama cha mapinduzi kwa zaidi ya miaka kumi na tano akiwa katika uongozi wa nyadhafa mbalimbali katika chama chake.

Mwilinge alisema kwa sasa hawezi kueleza sababu iliyomfanya kuomba ridhaa ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa jimbo la Ismani huku akiahidi kuweka wazi vipaumbele vyake muda utakapofika.

Aidha Mwilinge alisema kuwa wananchama wa chama cha mapinduzi wanawajibu wa kujilinda chama hicho kwa kusimamia vizuri serikali na kusema mambo mazuri yanayofanywa na chama hicho.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: