Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali katika hafla fupi ya Uapisho wa Viongozi hao iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 16 Julai 2020.

Na Immaculate Makilika – MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wateule kwenda kutatua matatizo ya wananchi katika maeneo yao.

Akizungumza katika hafla ya kuapisha viongozi aliwateuwa hivi karibuni leo Alhamisi (Julai 16, 2020) Ikulu, Chamwino Dodoma, Rais Magufuli aliwataka viongozi wateule kwenda kufanyakazi, kusimamia shughuli za maendelo pamoja na kutatua matatizo ya wananchi ikiwemo migogoro mbalimbali huku akitolea mfano mgogoro wa ardhi wa ulipo katika Wilaya ya Chunya, jinini Mbeya.

“Mkatimize wajibu wenu na kufanyakazi vizuri, mkamtangulize Mungu katika shughuli zenu na mkawatumikie watanzania na hasa wananchi masikini waliopo katika maeneo yenu,” alisema Rais Magufuli

Aidha, Rais Magufuli alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Maduhu Isaac Kazi ambaye ni kati ya viongozi aliowateua kuhakikisha kuwa hakuna urasimu katika kuwawezesha wawekezaji kutekeleza miradi yao hapa nchini.

“Tusiwazungushe wawekezaji, tuwavutie waje kuwekeza nchini, nchi yetu ina maeneo mbalimbali ya uwekezaji ikiwemo Kigamboni na Kibaha, tuongeze kasi katika utendaji wetu ili tuendelee kujenga uchumi wetu, na sasa tumeingia uchumi wa kati basi tujitahidi zaidi” alisisitiza Rais Magufuli

Kwa upande, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliwapongeza wateule wapya na kuwataka kuwa watumishi wa watu badala ya kuhaha na madaraka waliyoyapata.

Viongozi walioapishwa ni pamoja na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa maeneo mbalimbali na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),ambao waliteuliwa katika nafasi hizo hapo jana Julai 15, 2020.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: