Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimzawadia kofia msanii Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platinumz baada ya kutumbuiza maelfu kwa maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Jumatatu Septemba 7, 2020
Na Said Mwishehe,Michuzi TV- Mwanza

MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli ameonesha upendo mkubwa kwa msanii Naseeb Abdull a.k.a Diamond kwa kuamua kuvua kofia yake aliyovaa na kisha kumvalisha msanii huyo.

Tukio ambalo lilifanyika mbele ya maelfu ya wakazi wa Mwanza lilisababisha kuibuka kwa shangwe kutoka kwa mashabiki wa muziki na hasa muziki wa kizazi kipya maarufu kwa jina la Bongo.

Diamond alikuwa moja ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya na baada kufika katika Uwanja huo ambao idadi ya watu ilikuwa kubwa sana, alipewa nafasi ya kutumbuiza ambapo aliimba nyimbo tatu.

Msanii huyo kama kawaida yake alionesha umahiri wake wa kuimba,kucheza na kutawala jukwaa, hivyo maelfu ya wananchi waliokuwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika mkutano walikuwa wakishuhudia mtoto wa Tandale akifanya vitu vyake mbele ya Rais.

Hata hivyo baada ya kumaliza kutumbuiza Diamond aliwashakuru wana Mwanza kwa kufika kwenye mkutano huo na wakati anataka kuanza kushuka kwenye jukwaa ndipo sasa Rais Magufuli akamuita meza kuu alikokuwa amekaa.

Baada ya kufika meza kuu, Dk.Magufuli Magufuli alisimama na kisha kutoa kofia yake kichwani na kumvalisha Diamond ,jambo ambalo hakuna aliyelitarajia kama litatoke lakini kwa Dk.Magufuli ambaye amekuwa akiwaependa wasanii aliona anayo nafasi ya kumzawadia kofia yake.

Diamond alipopewa kofia alishuka jukwaa kuu alilokuwa amekaa Dk.Magufuli huku akionekana kuwa na furaha baada ya kupewa kofia na Rais.

Hata hivyo baadae kupitia mitandao ya kijamii Diamond alionekana kupitia akaunti ya instagram akiiweka kofia hilo kwenye kabati lake ambalo anatunza tuzo zake ambazo amekuwa akipewa kutokana na sanaa yake ya muziki.

Hata hivyo wakati anaingia uwanjani hapo ,Dk.Magufuli na viongozi wengine walikuwa wameshafika na wakati anaingia uwanja ulizizima kwa shangwe katika maeneo aliyokuwa akipita kiasi cha kwamba aliyekuwa akizungumza kwa wakati huo kutosikika vizuri.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: