Nahodha wa timu ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Ally Samata (katikati) akiwa ameshatia saini kandarasi ya miaka minne ya kukitumikia kikosi cha Fenerbahnce kilichopo nchini Uturuki kwa euro milioni 8 akitokea Aston villa inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza.

MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta rasmi amesaini kandarasi ya miaka minne na kujiunga na miamba ya jiji la Istanbul, Fenerbahce akitokea Aston villa kwa dau ya euro milioni 8.

Klabu ya Fenerbahce imethibitisha rasmi kuinasana saini ya mshambuliaji huyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii za Instagram na Twitter.

Klabu ya Aston villa, kupitia ukurasa wake wa Instagram imemtakia kila la heri nyota huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania katika maisha mapya ya soka akiwa Fenerbahce.

Samatta alijiunga na Aston villa Januari mwaka huu akitokea Genk ya ubeligiji kwa dau la Paundi milioni 10.

Samatta amekuwa hana wakati mzuri katika kikosi cha Aston villa chini ya kocha Dean Smith, na kupelekea kutopata nafasi katika kikosi cha kwanza, katika msimu mpya ulioanza Semptemba 12. 

Inaelezwa kuwa huenda ujio wa Ollie Watkins kutoka Brentford, ikawa sababu ya Samatta kuondoka villa park.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: