Na Amiri Kilagalila, Njombe

SERIKALI Wilayani Njombe imeongeza muda wa siku nne kuanzia leo za kutuma maombi kwa ajili ya kujiunga na nafasi za jeshi la kujenga Taifa (JKT) kutokana na vijana kutojitokeza kwa wingi mwaka huu.

Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri amesema zoezi hilo lilitakiwa kukamilika septemba 9 mwaka huu na kutokana na idadi ndogo ya vijana waliokwenda kuomba, serikali imeongeza muda huo wa siku nne hadi tarehe 11.

“Tarehe yetu ya mwisho ya kupokea tulikuwa tumepanga iwe tarehe 9 saa kumi jioni ambayo ni kesho,lakini mimi nimefungua na nitaendelea kupokea majina ya waombaji wote na vikao vyangu nitafunga rasmi tarehe 11”alisema Ruth Msafiri.

Aidha Bi.Msafiri amesema vijana wenye sifa ya kujiunga na JKT ni wenye elimu ya darasa la saba hadi chuo kikuu ambapo vijana 130 wanahitajika kujiunga na jeshi hilo.

“Kwa kuwa lengo ni kupata vijana wa kutosha kupata fani na stadi mbali mbali za maisha,hii inahusisha madarasa yote kwa maana elimu ya msingi,sekondari,kidato cha sita, cheti, lakini pia hata wa chuo kikuu”aliongeza DC Msafiri.

B.Msafiri ametumia fursa hiyo kukemea tabia za baadhi ya watu wanaotaka kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia zoezi hilo kinyume na sheria ambapo kwa atakaye bainika hatua kali zitachukuliwa.

“Hizi nafasi hazitolewa kwa upendeleo wa aina yeyote,wewe ukitoa rushwa utakuwa umeumizwa,mimi sitoi hiz nafasi kwa upendeleo kwasababu sio za mfukoni ila tunakwenda nazo kwa sifa”alisema Ruth Msafiri
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: