Diwani viti maalum manispa ya Ilala Batuli Mbaraka Mziya akizindua saloon pamoja na kiwanda kidogo cha vipodozi kinachomilikiwa na mtoto wa Masaburi kilichopo Tabata na Mikocheni jijini Dar es salaam.

Vicent Macha Dar es salaam

Vijana wanaokabiliwa na changamoto za mitaji kote nchini wametakiwa kuunda vikundi vya watu watano, kumi au zaidi ili kuweza kupata mikopo ya halmashauri ambayo ni asilimia 10 iliyotengwa kwa ajili ya vijana, wanawake na walemavu.

Hayo yameelezwa na Diwani wa viti maalum Manispaa ya Ilala Mh. Batuli Mbaraka Mziya alipoalikwa kuzindua saloon pamoja na kiwanda kidogo cha vipodozi cha Dote Naturelz Court kilichopo Tabata pamoja na Mikocheni jijini Dar es salaam.

Mh. Batuli amesema kuwa Chuchu Dote amekuwa mfano wa kuigwa na jamii kwani ameitekeleza sera serikali ya awamu ya tano kwa vitendo ya kuanziasha viwanda, Kwani amejipambanua kuwa mzalendo wa kweli kwa kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli.

Ameongeza kuwa vijana wengi waachane na dhima ya kusubiri kuajiliwa na matokeo yake wawekeze nguvu zao katika kujiajiri kama ilivyo kwa Chuchu Dote leo, Kwani amehitimu degree yake na kaamua kuachana na mambo ya kutafuta ajira na kuamua kujiajiri na kuweza kutoa ajira kwa vijana wenzake. 

Aidha ameedelea kusisitiza kuwa bidhaa za Chuchu Dote ni nzuri kwani ni za asili na azichubui Ngozi bali zinaimarisha na kuifanya Ngozi yako iwe nzuri, pia amependa kuwasihi wakina mama pamoja na wakina baba kutumia bidha hizo kwani hazina kemikali zozote na zinafaa kwa watu wa aina zote

Kwa upande wake mmiliki wa Dote Naturalz court Chuchu Dote amesema kuwa kwa Tanzania atakuwa ni msanii wa kwanza wa vichekesho vya jukwani (stand up comedy) kuweza kumiliki kiwanda kidogo na pia kuwa na mfanikio makubwa kama haya.

Aidha amesema changamoto kubwa kwa Tanzania ni kwamba watu wakisikia vitu vya asili mawazo yao uja kwa watu weusi tu,

“Kwani mtu unapomwambia bidhaa hii ni asili anakwambia hivyo ni vitu vya watu weusi na siyo kwa sisi weupe na wanasahau kuwa unaweza kuwa mweupe na ukawa natural kwa kutopaka vitu vyenye kemikali, hiyo ndio shida kubwa kwa wateja wetu wengi”. Amesema Chuchu Dote

Bidhaa zinazotengenezwa na Dote Naturalz ni mafuta ya nywele, mafuta ya ngozi (lotion), shampuu za nywele na sabuni. Na vyote ni vya asili vinatengenezwa na vitu vya asili kama maji ya madafu, nazi, parachichi n.k

Ameendelea kuwasisitiza watanzania wote kutumia bidhaa za Chuchu Dote kwani zinasaidia kufanya Ngozi iwe nyororo na nadhifu pamoja na mafuta ya dote yanasaidia kukuza nywele na kuzipa muonekano mzuri.

Na mwisho amewataka vijana kujituma ili kuweza kufikia mafanikio wanayoyataka lakini pia kujikita katika ubunifu ili kuimarisha uchumi wa nchi yetu na kumsaidia Rais wetu katika kukuza na kuinua sekata ya viwanda.
Diwani wa viti maalum manispaa ya Ilala Mh. Batuli Mbaraka Mziya akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa uzinduzi wa kiwanda kidogo cha Dote Naturalz Court kinachomilikiwa na mtoto wa marehemu Didas Masaburi
Wageni wakifuatilia shughuli ya uindui wa Dote Natural Court.
Mkurugenzi wa Dote Naturalz Court, Chuchu Dote Masaburi akionesha baadhi ya bidhaa zinzotengenezwa katika kiwanda chake kilichopo Mikocheni na Tabata jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji na mmiliki wa wa Dote Naturalz Court Chuchu Dote Masaburi akielezea baadhi ya bidhaa zinazopatika katika kiwanda chake mapema jana jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Dote Naturalz akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa waliofika katika shughuli hiyo ya uzinduzi Dote Naturalz Court
Baadhi ya bidhaa zinazopatikana Dote Naturalz Court
Muonekano wa logo ya dote natural court
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: