Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jocate Mwegelo(kushoto) akiwa na Msanii maarufu katika muziki wa Bongo Fleva Nasseb Abdull 'Diamond' baada ya kumkabidhi fulana yenye jina lake kuelekea Kisarawe Ushoroba Festival kuanzia Machi 5 hadi Machi 7 mwaka huu.Diamond ni miongoni mwa wasanii wakubwa watakaokuwepo kwenye tamasha hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jocate Mwegelo(wa tatu kushoto) akizungumza na wananchi wa Wilaya ya hiyo kuelekea Kisarawe Ushoroba Festival ambalo litafanyika kuanzia Machi 5 hadi Machi 7 mwaka huu. Wa pili kulia ni msanii Nasseb Abdull maarufu kwa jina la Diamond ambaye ni miongoni mwa wasanii watakaokuwepo katika tamasha hilo.Wengine kwenye picha hiyo ni viongozi wa wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jocate Mwegelo akiwa na msanii Diamond Platnumz wakielekea kwenye uwanja wa Chanzige ambapo tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival litafanyika kuanzia Machi 5 hadi Machi 7 mwaka huu.
Msanii Diamond Platnumz (wa pili kulia) akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kisarawe kuekelea Kisarawe Ushoroba Festival.(wa tatu kushoto) ni Mkuu wa Wilaya hiyo Jocate Mwegelo. Wengine ni baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jocate Mwegelo akiwa na Msanii Nasseb Abdull 'Diamond' baada ya kutembelea moja ya maeneo ya vivutio vya utalii vilivyopo katika wilaya hiyo. Diamond amekwenda kwenye wilaya hiyo leo kuangalia maandalizi ya kuelekea Kisarawe Ushoroba Festival.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jocate Mwegelo akizungumza na msanii Nasseb Abdull 'Diamond' hayuko pichani, baada ya msanii huyo kufika katika ofisi za mkuu huyo wa wilaya ikiwa ni maandalizi kuelekea Kisarawe Ushoroba Festival.

Msanii Diamond Platnumz akiwasalimia mashabiki wake baada ya kufika kwenye ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.
Msanii Nasseb Abdull 'Diamond' akinunua matunda baada ya kutembelea soko la Kisarawe kuelekea tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: