Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mfanyabiasha Bw. Christopher Kontonasios wa Kampuni ya ZANCHICK, wakati wa mkutano wake na Wafanyabiasha wanaoagiza bidhaa za vyakula kutoka Nje, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar,Mhe. Omar Said Shabaan.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shabaan akifuatilia mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) wakati akizungumza na Wafanyabiashara waagiziaji wa Vyakula kutoka Nje, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Mfanyabiashara wa kampuni ya Sab-Sahara Zanzibar Bw. Ali Salum Ali akizungumza na changia wakati wa mkutano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar kuelezea changamoto zao katika uagizaji wa bidhaa kutoka nje.
Mfanyabiashara wa Kampuni ya Bopar Enterprises Zanzibar Bw. Said Nassir Bopar akizungumza na kuchangia wakati wa mkutano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) na kuwataka Wafanyabiashara kuwa na ushirikiani na katika biashara zao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa za Vyakula kutoka nje, akjisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na wafanyabiashara uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na (kulia kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shabaan.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Bw.Nahat Mohammed Mahfoudh akizungumza na kutoa ufafanuzi wakati wa mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa mkutano wake na Wafanyabiashara wanaoagiza Vyakula kutoka nje, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
(Picha na Ikulu)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: