Na Thadei Ole Mushi.

Mkurugenzi wa Air Tanzania amesema kuwa ni kweli kuwa ndege yetu imesukumwa kurudi nyuma katika uwanja wa Ndege wa Zanzibar baada ya Rubani kuingia kwenye Runway iliyokuwa imefungwa.

Kwa Mujibu wa maelezo yake ni kuwa Uwanja wa Zanzibar hauna magari maalum ya kusukuma ndege kurudi nyuma.

TUJIFUNZE.

Kitendo cha kusukuma ndege kurudi nyuma ni cha kawaida kabisa pindi inapolazimu kufanywa hivyo.

Kitendo hiki huitwa "Aviation Pushback" kitaalamu na kwa lugha ya wenzetu hutafsiriwa hivi:-

Aviation, pushback is an airport procedure during which an aircraft is pushed backwards away from an airport gate by external power.

Pushbacks are carried out by special, low-profile vehicles called pushback tractors or tugs.

Kwa nini husukumwa kwa kutumia External power?

Ndege husukumwa Kurudi nyuma kwa kutumia nguvu toka njee kuepuka kuleta madhara kwenye engine. Si kwanba ndege haiwezi kurudi nyuma yenyewe lah Hasha Ila kitaalamu ukitumia gia kuirudisha nyuma huleta madhara makubwa kwenye engine.

Kuna mlolongo wa sababu:-

√. Ndege hurudishwa nyuma kwa External power kuepuka makelele ya engine.

å Hurudishwa nyuma kwa kutumia External power kwa sababu Pilot anakuwa haujui uwanja vizuri kama anavyoujua dereva wa Tugs au Tractor.

å Hurudishwa nyuma kwa kutumia External power kwa Sababu dereva wa Tugs anauwezo wa kuona mazingira yanayozunguka ndege si rahisi kwa rubani kuona nyuma.

å Ni njia nzuri ya kubana matumizi ya mafuta.

å Ni njia nzuri ya kuzuia uharibifu wa engine kwa kuwa kitendo cha kurudisha nyuma kwa kutumia gia engine hufyonza mchanga.

Fuata link link hii kujifunza zaidi...


Ndege zetu ni nzima kabisa na Mkurugenzi kathibitisha hilo.

Tuwe mabalozi wazuri wa Mali zetu wenyewe. Tusiwajengee hofu abiria wanaotumia shirika letu la ndege.

Faida inayopatikana ATCL ndio inayotulipa mishahara sisi wafanyakazi, ndio inayonunua madawa, ndiyo inayo tengeneza mabarabara na ndiyo inatumika kutoa Elimu Bure.

Tunaweza kuendelea kupingana kwa itikadi Ila si kuhujumu maendeleo yetu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: