Articles by "MICHEZO"
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
KILOLO, IRINGA, 31 Oktoba 2026: Benki ya Exim Tanzania imeendelea kudhihirisha dhamira yake ya kushirikiana na jamii katika kuchochea maendeleo endelevu kupitia udhamini wake Mkuu wa Kitonga Marathon 2026, mbio zilizolenga kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kutangaza fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.

Mbio hizo zilizofanyika chini ya kaulimbiu “Tunza Mazingira, Wekeza Kilolo” ziliwakutanisha washiriki na wadau mbalimbali kwa lengo la kuhamasisha utunzaji wa mazingira, ushiriki wa jamii na kuangazia fursa za maendeleo zilizopo wilayani humo, ikiwemo katika sekta za kilimo, utalii na biashara za wenyeji.

Kama Mdhamini Mkuu, Benki ya Exim iliunga mkono mbio hizo kama sehemu ya dhamira yake pana ya kushirikiana na jamii na wadau katika masuala yanayochangia maendeleo endelevu.Akizungumzia udhamini huo, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu, alisema udhamini huo unaakisi imani ya Benki kwamba jukumu lake haliishii katika kutoa huduma za kifedha pekee, bali linajumuisha pia kuunga mkono mipango inayowaunganisha wadau katika kutekeleza vipaumbele vya pamoja vya maendeleo.

“Mbio za Kitonga zinatoa fursa ya kuitangaza zaidi Kilolo na uwezo wake wa kiuchumi, huku zikihamasisha uwajibikaji wa pamoja katika uhifadhi wa mazingira. Sisi Exim Bank tunaamini kuwa maendeleo endelevu yanahitaji ushirikiano kati ya jamii, wafanyabiashara na wadau wengine. 

Udhamini wetu wa mbio hizi unaakisi dhamira yetu ya kushirikiana na jamii tunazozihudumia na kuchangia juhudi zinazolenga kuleta maendeleo katika maeneo yao,” alisema Kafu.

Udhamini huo ni sehemu ya jitihada za Benki ya Exim Tanzania za kuchangia maendeleo ya jamii kupitia mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii, Exim Cares. Kupitia mpango huo, Benki inaunga mkono shughuli mbalimbali zinazolenga kuboresha maisha ya jamii katika sekta za afya, elimu, uhifadhi wa mazingira, ubunifu na elimu ya masuala ya fedha.

Mwaka 2026, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 29 tangu kuanzishwa kwake, Benki ya Exim ilifanya shughuli za usafi katika jamii zinazozunguka matawi yake nchini. Mkoani Iringa, timu ya tawi la Benki hiyo ilikabidhi vifaa vya usafi katika Hospitali ya Wilaya ya FLERIMO ili kusaidia kuboresha usafi katika hospitali hiyo.

Benki ya Exim Tanzania ilifungua tawi lake mkoani Iringa mwaka 2009. Tawi hilo hutoa huduma za kifedha kwa watu binafsi, wafanyabiashara, kampuni na taasisi, kulingana na mahitaji yao. Ushiriki wa tawi hilo katika Mbio za Kitonga unaonyesha namna Benki inavyoendelea kushirikiana na jamii inayohudumia pamoja na wadau wengine katika kuunga mkono mipango inayochangia maendeleo ya mkoa huo.

Kupitia Tawi lake la Iringa, Benki ya Exim Tanzania inaendelea kuwahudumia watu binafsi, wafanyabiashara na kampuni kwa kuwapatia huduma mbalimbali za kifedha. Wakazi na wamiliki wa biashara mkoani humo wanaweza kutembelea tawi hilo kupata maelezo kuhusu bidhaa na huduma za Benki, pamoja na ushauri kuhusu huduma zinazoweza kukidhi mahitaji yao ya kifedha.

Na Mwandishi Wetu.

Dar es Salaam-Tanzania, 9 Oktoba 2026: Kombe la Ligi Kuu ya Uingereza limewasili Tanzania, kwa mara ya kwanza, likiashiria kuanza kwa ziara yake ya Afrika Mashariki. Kombe hilo limeletwa na bia ya Guinness, ambayo ni mmoja wa wadhamini wa vinywaji wa Ligi Kuu hiyo kubwa ya soka duniani.

Kuwasili kwa Kombe hilo kunaashiria kuanza kwa sherehe za siku mbili zitakazounganisha hadhi ya Ligi Kuu ya Uingereza na utamaduni wa soka Tanzania.

Kwa Guinness, kuwasili kwa Kombe hili si suala la kuleta tu moja ya alama zinazotambulika zaidi katika soka duniani, ni kutengeneza tukio ambalo linaunganisha soka la kimataifa na mapenzi, nguvu na utamaduni wa soka la Tanzania.

Kuhusu ujio huo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Serengeti Breweries Dk. Obinna Anyalebechi alisema:

“Ligi Kuu ya Uingereza tayari ina nafasi kubwa katika mioyo na mazungumzo ya mamilioni ya mashabiki wa soka, wakiwemo Watanzania. Kinachofanya tukio hili kuwa tofauti ni kwamba sasa Kombe lenyewe limefika hapa, likikutana na mashabiki mahali ambapo mapenzi yao kwa soka yanaishi. Tunataka kuandaa tukio ambalo lina ladha ya Tanzania na kuipa dunia nafasi ya kuona kinachotokea pale soka la kimataifa linapokutana na nguvu, ubunifu na mapenzi yetu wenyewe kwa mchezo huu.”
 
Kuwasili kwa Kombe hilo pia kumeingia moja kwa moja kwenye utamaduni mkubwa wa soka nchini, huku mashabiki wa Simba SC na Young Africans (Yanga) wakiwa sehemu ya hamasa hiyo. Klabu hizi mbili ni miongoni mwa makundi makubwa zaidi ya mashabiki nchini, huku wengi wao pia wakifuatilia kwa karibu Ligi Kuu ya Uingereza.

Mkurugenzi wa Masoko na Ubunifu wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Henry Esiaba alisema:

“Tanzania ina utamaduni mkubwa sana wa soka, na kulileta Kombe la Ligi Kuu ya Uingereza hapa kumetupa nafasi ya kuona mapenzi hayo kwa karibu. Tanzania ikiwa sehemu ya safari hii ya Afrika Mashariki, tunataka Kombe hili liwe sehemu ya tukio halisi la soka la Tanzania tukio hili liongozwe na mashabiki, simulizi zao na namna wanavyosherehekea ujio wa Kombe hili na mchezo wa soka kwa ujumla.”

Kwa jamii ya soka Tanzania, tukio hili pia linaunganisha utamaduni unaokua wa soka nchini na ulimwengu mpana wa soka la kimataifa.
Mwakilishi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Aaron Nyanda alisema:

“Kuwasili kwa Kombe la Ligi Kuu ya Uingereza kunaonyesha uhusiano mkubwa uliopo kati ya jamii yetu ya soka na soka la kimataifa. Kuanzia hamasa inayozunguka klabu zetu hadi Ligi Kuu ya Uingereza na mashindano ya kimataifa, mashabiki wa Tanzania wanafuatilia soka katika ngazi mbalimbali. Tukio hili linaunganisha mapenzi hayo na kuwapa mashabiki wetu nafasi ya kukutana na soka la kimataifa kwa namna tofauti.”

Umuhimu wa tukio hili unaenda zaidi ya soka, kwa kuunganisha michezo, burudani, utamaduni na vijana, huku Tanzania ikipata nafasi ya kuionyesha dunia mapenzi na utamaduni wake wa soka.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, aliyehudhuria tukio hilo alisema:“

Michezo huwaleta watu pamoja, hutengeneza fursa kwa vijana na kutoa nafasi kwa nchi kuonyesha utamaduni na utambulisho wake. Kwa hiyo, kuwasili kwa Kombe la Ligi Kuu ya Uingereza si tukio kwa mashabiki wa soka pekee, bali pia ni fursa ya kuonyesha nafasi kubwa ambayo michezo inaendelea kuwa nayo katika jamii yetu.”

Baada ya Tanzania, Kombe hilo litaendelea na safari yake nchini Uganda tarehe 11 hadi 13 Oktoba na kumaliza safari yake nchini Kenya.
Mashabiki wa Ligi Kuu ya England nchini Tanzania wanajiandaa kushuhudia tukio la kipekee baada ya Kombe la Ligi hiyo kutua rasmi nchini kwa mara ya kwanza kupitia Guinness, Mdhamini Mkuu wa Bia wa Ligi Kuu ya England.

Kombe hilo litawasili nchini Ijumaa, Oktoba 9, 2026, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) majira ya saa tatu asubuhi, kabla ya kuzungushwa katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam ili kuwapa mashabiki fursa ya kuliona kwa karibu.

Hivyo, kwa mashabiki wa EPL ambao wamezoea kuliona Kombe hilo likikabidhiwa baada ya msimu kumalizika kupitia televisheni, safari hii litakuwa mbele yao na katika jiji lao.Baada ya kuzunguka katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, Kombe hilo litahamia The Super Dome, Masaki, ambako kutakuwa na hafla maalum kwa wageni na mashabiki kupata fursa ya kuliona kwa karibu zaidi na kupiga picha nalo.
Akizungumzia ujio wa Kombe hilo, Mkurugenzi wa Ubunifu na Masoko wa Serengeti Breweries Limited (SBL), Henry Esiaba, alisema Guinness inaleta uzoefu wa EPL karibu zaidi na mashabiki wa soka nchini.

“Mashabiki wa Tanzania wana mapenzi makubwa na Ligi Kuu ya England na kila wiki wanafuatilia mechi, wanajadili timu zao na kusherehekea pamoja. Safari hii tunataka kuwapa nafasi ya kuona Kombe lenyewe kwa karibu na kuwa sehemu ya tukio hili. Ni fursa kwa mashabiki kupata uzoefu tofauti na ule wanaoupata wanapotazama mechi kwenye televisheni,” alisema Esiaba.

Burudani ya soka itaendelea Jumamosi, Oktoba 10, ambapo mashabiki watakutana katika Uwanja wa KMC, Mwenge, kwa Guinness Matchday.
Katika tukio hilo, mashabiki watapata fursa ya kushuhudia kwa pamoja mechi za Ligi Kuu ya England kupitia skrini kubwa, ikiwemo mchezo wa Arsenal dhidi ya Leeds pamoja na Manchester United dhidi ya Tottenham Hotspur.

Lakini kwa kuwa soka Tanzania lina ladha yake, siku hiyo pia mashabiki watapata nafasi ya kushuhudia Dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga mubashara kupitia skrini kubwa zitakazowekwa katika eneo la tukio.

Hiyo itakuwa fursa ya mashabiki wa soka kukutana sehemu moja, kufuatilia mechi za Ligi Kuu ya England na wakati huo huo kushuhudia moja ya mechi zinazovuta hisia kubwa zaidi katika soka la Tanzania.Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kampuni wa SBL, Juanita Mramba, alisema ujio wa Kombe hilo unalenga kuwaleta pamoja mashabiki na wadau wa soka kupitia uzoefu unaounganisha soka la kimataifa
“Soka linawajumuisha watu wengi na Tanzania ni moja ya nchi ambazo mashabiki wake wanaishi kwa karibu sana na mchezo huu. Kupitia ujio wa Kombe la EPL, tunataka mashabiki wapate nafasi ya kuliona kwa macho yao, kupiga picha nalo na kushiriki katika matukio yatakayowakutanisha pamoja. Hii ni nafasi ya kusherehekea soka na mashabiki ambao wamekuwa sehemu muhimu ya utamaduni wa mchezo huu,” alisema Juanita.

Mbali na kutazama mechi, mashabiki watakaohudhuria Guinness Matchday watapata pia fursa ya kupiga picha na Kombe la Ligi Kuu ya England, huku wakifurahia burudani na mazingira ya pamoja ya kusherehekea soka.Ujio wa Kombe hilo Tanzania unaifanya Dar es Salaam kuwa sehemu ya ziara maalum ya Kombe la Ligi Kuu ya England katika Afrika Mashariki, huku Guinness ikiendelea kutumia nafasi yake kama Mdhamini Mkuu wa Bia wa Ligi hiyo kuwaleta mashabiki karibu na mchezo wanaoupenda.

Kwa siku mbili, Oktoba 9 na 10, macho ya mashabiki wa soka yataelekezwa Dar es Salaam, kuanzia ujio wa Kombe hilo JNIA, safari yake katika maeneo mbalimbali ya jiji, hafla ya Super Dome Masaki hadi Guinness Matchday katika Uwanja wa KMC, Mwenge.Kwa mashabiki wa EPL na soka kwa ujumla, hii ni nafasi ya kuliona Kombe la Ligi Kuu ya England kwa karibu na kusherehekea soka pamoja na mashabiki wengine.
Mkurugenzi wa Vodacom Business wa Vodacom Tanzania PLC, Nguvu Kamando (kushoto), akikabidhi tuzo kwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya Vodacom Coastal Classic upande wa wanawake, Mary Aleper (katikati) kutoka Uganda. Washindi wengine wa mashindano hayo walikuwa Ditona Munu Martinie mshindi wa pili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) (wa pili kushoto) na Mercy Elegae kutoka Kenya, aliyeshika nafasi ya tatu.

Washindani wa mashindano ya Vodacom Coastal Classic wakiwa katika eneo la kuanzia mashindano hayo kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, kuelekea Bagamoyo, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Tehama wa Vodacom Tanzania Plc Athumani Mlinga.

Mshindi wa Kwanza wa Mashindano ya Vodacom  Coastal Classic upande wa wanaume Charles Kagimu kutoka Uganda (katikati) mshindi wa pili Jordan Schleck kutoka Uganda (kushoto) na mshindi wa tatu Boniphace Ngwata kutoka Tanzania (kulia), wakionesha mfano wa hundi walizokabidhiwa katika mashindano hayo. Washindi hao walijishindia milioni 10 kwa mshindi wa kwanza, milioni 7 kwa mshindi wa pili, na milioni 5 kwa mshindi wa tatu mtawalia.
Washiriki wa Mashindano ya Nyerere Cycling Tour wakiendelea na Mashindano hayo ukanda wa Pwani wa bahari ya Hindi kuelekea Bagamoyo.
Mkurugenzi wa Vodacom Business kutoka Vodacom Tanzania PLC Nguvu Kamando (kulia), na mwanzilishi wa msafara wa baiskeli wa Nyerere Cyling Tour Gabriel Landa kushoto, wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa mashindano wa Cycling Tour Upande wa wanawake, Mary Aleper kutoka Uganda aliyeshika nafasi ya kwanza (katikati), Ditona Munu Martinie kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) aliyeshika nafasi ya pili (wa pili kushoto), na Mercy Elegae kutoka Kenya aliyeshika nafasi ya tatu (wa pili kulia). Washindi hao walijishindia kiasi cha shilingi milioni 10, milioni saba na milioni tano kila mmoja.

Na Mwandishi Wetu.

Bagamoyo, Pwani - 4 Oktoba 2026: Uzinduzi wa mashindano ya Vodacom Coastal Classic umeonesha namna ambavyo michezo inaweza kuwa chachu ya kukuza utalii, elimu na maendeleo ya jamii, huku mashindano hayo ya kuendesha baiskeli yakitoa fursa ya kuonesha vivutio vya utalii vilivyopo katika ukanda wa pwani ya Tanzania na kuunga mkono shughuli zenye manufaa ya muda mrefu kwa jamii ambazo msafara wa waendesha baiskeli wa Nyerere Cycling Tour (zamani Twende Butiama) utapita.

Kwa kuwakutanisha waendesha baiskeli, jamii na wadau mbalimbali, mashindano hayo yametoa mchango katika kukuza utalii wa ndani, kuhamasisha vijana kupitia michezo na kusaidia jitihada za elimu na maendeleo katika maeneo yanayounganishwa na safari hiyo.Mashindano hayo, ambayo ni sehemu ya maandalizi kuelekea msafara wa Nyerere Cycling Tour, yaliwakutanisha waendesha baiskeli 147 walioshiriki mbio hizo zilizopita katika maeneo ya kuvutia ya ukanda wa pwani ya Tanzania. Mbali na kutoa ushindani kwa waendesha baiskeli, mashindano hayo yameendelea kuonesha fursa za utalii nchini na kuongeza uelewa kuhusu shughuli za elimu, afya na uhifadhi wa mazingira zitakazotekelezwa katika maeneo mbalimbali wakati wa safari ya msafara huo kuelekea Butiama.

Afisa Mwandamizi wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Charles Maguzu aliwapongeza waandaaji na washiriki wa mashindano hayo kwa kutumia michezo kama jukwaa la kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi, huku ikiendelea kuimarisha nafasi ya Tanzania kama kituo cha utalii wa michezo.

“Vodacom Coastal Classic ni ushahidi wa namna mchezo wa baiskeli unavyozidi kuwa na nafasi muhimu katika kuhamasisha maisha yenye afya, kutoa fursa kwa vijana wenye vipaji na kuonesha vivutio vya utalii vya Tanzania. Kupitia matukio kama haya, hatuendelezi vipaji vya michezo pekee, bali pia tunachangia katika elimu, uelewa kuhusu uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya jamii. Tunawapongeza Vodacom na washirika wote kwa kuendelea kuwekeza katika kukuza mchezo huu na kuhamasisha kizazi kijacho cha waendesha baiskeli,” alisema.

Baada ya ushindani mkali, Charles Kagimu Kutoka Uganda na Mary Aleper kutoka Uganda waliibuka washindi wa mashindano ya Vodacom Coastal Classic 2026 baada ya kumaliza katika nafasi ya kwanza kwa upande wa wanaume na wanawake, ambapo kila mmoja alizawadiwa shilingi milioni 10.Mashindano hayo yaliwapa waendesha baiskeli fursa ya kutumia vipaji vyao kama chanzo cha kipato kupitia ushindani wa kitaaluma, huku yakihamasisha vijana zaidi kushiriki katika mchezo huo.

Washindi wa nafasi ya kwanza katika kila kundi walipata shilingi milioni 10, huku washindi wa nafasi ya pili wakipata shilingi milioni 7 na nafasi ya tatu shilingi milioni 5. Waendesha baiskeli waliomaliza katika nafasi ya nne hadi ya kumi katika kila kundi walizawadiwa shilingi milioni 1 kila mmoja.

Akizungumza baada ya mashindano hayo, Mkurugenzi wa Vodacom Business wa Vodacom Tanzania PLC Nguvu Kamando, aliwapongeza washindi pamoja na waendesha baiskeli wote walioshiriki, akieleza kuwa mashindano ya Vodacom Coastal Classic yataendelea kutoa fursa kwa waendesha baiskeli kuonesha vipaji vyao huku yakichangia katika malengo mapana ya maendeleo ya taifa.

“Zaidi ya ushindani wenyewe, Vodacom Coastal Classic na Nyerere Cycling Tour zinasaidia kukuza utalii wa ndani, kuunga mkono shughuli za elimu na kuhamasisha matokeo chanya ya kijamii katika jamii zinazopitiwa na safari hii. Tunajivunia kuwa sehemu ya jukwaa linalowawezesha vijana, wakiwemo wasichana, huku likitumia michezo kama nyenzo ya kuchochea maendeleo,” alisema.

Kwa upande wake, Meneja wa Uendelevu wa Stanbic Bank Tanzania, Annette Nkini, alisema ushirikiano huo unaonesha dhamira ya benki hiyo katika kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi hapa nchini.

“Kwa miaka 30, Tanzania imekuwa zaidi ya soko kwa Stanbic Bank; ni nyumbani kwetu. Vodacom Coastal Classic na Nyerere Cycling Tour vinaonesha uwezo wa Tanzania katika utalii, vinawekeza katika elimu na vinafungua fursa kwa vijana na jamii kustawi. Kupitia ushirikiano huu tunawekeza kwa watu na jamii ambao maendeleo yao yataendelea kuijenga Tanzania ya kesho," alisema.

Aliongeza kuwa Stanbic Bank itaendelea kuunga mkono mashindano hayo kupitia ushirikiano wake katika Nyerere Cycling Tour na jitihada za kuhamasisha Watanzania wengi zaidi kushiriki mchezo wa baiskeli kama fursa ya michezo na uchumi.

Vodacom Coastal Classic ni sehemu ya shughuli zinazoambatana na Nyerere Cycling Tour, ambayo itahusisha safari ya kilomita 1,500 kutoka Dar es Salaam hadi Butiama kuanzia tarehe 5 hadi 14 Oktoba 2026. Safari hiyo itawakutanisha waendesha baiskeli kutoka Tanzania na nchi nyingine, sambamba na shughuli zinazolenga kuhamasisha elimu, afya na uhifadhi wa mazingira katika maeneo mbalimbali yatakayopitiwa.

Kampuni ya Vodacom Tanzania ndyo mshirika mkuu wa Nyerere Cycling Tour, huku Afro Oil, Stanbic Bank Tanzania, BYD, ABC, Coca-Cola na Huawei zikiwa miongoni mwa washirika wanaounga mkono mpango huo kwa ujumla.

Kumalizika kwa mashindano ya Vodacom Coastal Classic sasa kunaweka msingi wa kuendelea kwa safari ya Nyerere Cycling Tour, huku waendesha baiskeli wakijiandaa kuendelea na safari kuelekea Butiama, nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (Kulia) akikabidhi zawadi kwa mshindi wa jumla kwa upande wa wanaume Thomas Mwangi (kushoto) katika mashindano ya CEO Golf Tournament 2026, iliyofanyika Septemba 26, 2026 katika viwanja vya Sea Cliff Golf Course visiwani Zanzibar. Mashindano hayo yaliwakutanisha viongozi wa biashara, Maafisa Watendaji wakuu (CEOs), wanadiplomasia na wadau mbalimbali kutoka Tanzania na mataifa mengine ya Afrika, huku Vodacom Tanzania Plc ikiwa mdhamini mkuu wa tukio hilo lililolenga kuimarisha uhusiano, kujenga mitandao ya kibiashara na kukuza ushirikiano miongoni mwa viongozi wa sekta mbalimbali.
Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando akishiriki katika mashindano ya CEO Golf Tournament, iliyofanyika Septemba 26, 2026 katika viwanja vya Sea Cliff Golf Course visiwani Zanzibar. Mashindano hayo yaliwakutanisha viongozi wa biashara, Maafisa Watendaji wakuu (CEOs), wanadiplomasia na wadau mbalimbali kutoka Tanzania na mataifa mengine ya Afrika, huku Vodacom Tanzania Plc ikiwa mdhamini mkuu wa shindano hilo lililolenga kuimarisha uhusiano, kujenga mitandao ya kibiashara na kukuza ushirikiano miongoni mwa viongozi wa sekta mbalimbali.

Mkuu wa Masoko na Uwezeshaji wa Vodacom Business wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC Joseph Sayi (kulia) akikabidhiwa zawadi na afisa masoko wa kampuni hiyo Chelsea Njau, baada ya kuibuka mshindi wa Pili wa Mashindano ya CEO Golf Tournament 2026.
Mkuu wa idara ya Masoko na Uwezeshaji wa Vodacom Business katika kampuni ya Vodacom Tanzania PLC Joseph Sayi (kulia) akimkabidhi zawadi mshindi wa pili wa divisheni A katika Mashindano ya CEO Golf Tournament 2026, Ernest Sengeu (kushoto). Mashindano hayo yaliwakutanisha viongozi wa biashara, Maafisa Watendaji wakuu (CEOs), wanadiplomasia na wadau mbalimbali kutoka Tanzania na mataifa mengine ya Afrika, huku Vodacom Tanzania Plc ikiwa mdhamini mkuu wa shindano hilo lililolenga kuimarisha uhusiano, kujenga mitandao ya kibiashara na kukuza ushirikiano miongoni mwa viongozi wa sekta mbalimbali.
Mkuu wa Masoko na Uwezeshaji wa Vodacom Business katika kampuni ya Vodacom Tanzania PLC Joseph Sayi akishiriki katika mashindano ya CEO Golf Tournament. Mashindano hayo yaliwakutanisha viongozi wa biashara, Maafisa Watendaji wakuu (CEOs), wanadiplomasia na wadau mbalimbali kutoka Tanzania na mataifa mengine ya Afrika, huku Vodacom Tanzania Plc ikiwa mdhamini mkuu wa shindano hilo lililolenga kuimarisha uhusiano, kujenga mitandao ya kibiashara na kukuza ushirikiano miongoni mwa viongozi wa sekta mbalimbali.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuibuka na ushindi katika mashindano ya CEO Golf Tournament 2026, iliyofanyika Septemba 26, 2026 katika viwanja vya Sea Cliff Golf Course visiwani Zanzibar. Mashindano hayo yaliwakutanisha viongozi wa biashara, Maafisa Watendaji wakuu (CEOs), wanadiplomasia na wadau mbalimbali kutoka Tanzania na mataifa mengine ya Afrika, huku Vodacom Tanzania Plc ikiwa mdhamini mkuu wa shindano hilo lililolenga kuimarisha uhusiano, kujenga mitandao ya kibiashara na kukuza ushirikiano miongoni mwa viongozi wa sekta mbalimbali.

Na Mwandishi Wetu.

Vodacom Tanzania plc imeendelea kutumia mchezo wa golf kama jukwaa la kuunganisha viongozi wa biashara na makampuni, watoa maamuzi na wadau wa sekta mbalimbali, kupitia ushiriki na udhamini wake katika CEO Golf Tournament 2026, iliyofanyika Septemba 26 katika viwanja vya hotel Sea Cliff Golf Course, Zanzibar.

Mashindano hayo yamewakutanisha viongozi wa makampuni, maafisa watendaji wakuu (CEO’s), wanadiplomasia na wachezaji wa golf kutoka hapa nchini na mataifa mbalimbali ya Afrika ikiwemo Kenya, Uganda, Zambia, Malawi, Afrika Kusini na Nigeria, huku yakishirikisha zaidi ya wachezaji 80 kutoka mataifa hayo.

Wachezaji wa golf kutoka Kenya, Thomas Mwangi na Caroline Muigai, wametwaa ubingwa wa jumla kwa wanaume na wanawake mtawalia katika mashindano ya hayo yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania Plc.

Mwangi alitwaa ubingwa wa jumla kwa wanaume baada ya kukusanya pointi 40, huku Muigai akiibuka kinara kwa wanawake kwa pointi 41 katika mashindano yaliyochezwa kwa mfumo wa Stableford kwenye mashimo 18.

Katika Division A, Patrick O’Rourke alitwaa nafasi ya kwanza, huku Ernest Sengeu akimaliza wa pili kwa pointi 31.

Thagaran Govender alishinda Division B kwa pointi 39, akifuatiwa na Gregory Eayrs aliyepata pointi 38. Katika Division C, Abbas Simkoko alitwaa ushindi kwa pointi 40, akifuatiwa na Joseph Sayi aliyepata pointi 37.

Kwa upande wa wanawake, Salome Gakere alishinda kwa pointi 36, huku Vicky Elias akimaliza nafasi ya pili baada ya kufungana pointi 35 na Maryanne Mugo na kuamua kwa mfumo wa countback.

Ushiriki wa Vodacom Tanzania katika mashindano hayo umeenda zaidi ya mchezo wa golf na kuwa sehemu ya namna kampuni inavyotumia majukwaa ya michezo kujenga mahusiano na jumuiya ya biashara, huku ikiunganisha teknolojia na huduma za kidijitali katika mahusiano hayo kwa lengo la kuchochea ukuaji wa biashara.

Akizungumza wakati wa mashindano hayo, Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando, alisema kampuni hiyo inajivunia kuunga mkono mashindano yanayounganisha michezo na jamii ya wafanyabiashara.

“Tunafurahi kudhamini na kushiriki mashindano ya CEO Golf Tournament kwa sababu gofu si mchezo pekee, bali ni jukwaa linalowakutanisha watu, mawazo na fursa,” alisema Kamando.

Alisema mashindano hayo yanatoa mazingira rafiki kwa viongozi wa biashara kutoka sekta mbalimbali kukutana na kujenga mahusiano ya kikazi.
Kamando pia alihusisha mashindano hayo na juhudi za kukuza utalii visiwani Zanzibar, akisema matukio ya kimataifa ya michezo yanaitangza Zanzibar kwa wageni ambao wanaweza kurejea kwa ajili ya utalii au shughuli za kibiashara.

“Tunajivunia kushiriki katika kuitangaza Zanzibar kama kituo cha biashara, utalii na michezo. Matukio kama haya yanaongeza thamani si kwa washiriki pekee, bali pia kwa uchumi kiujumla,”alisema.

Hivyo, ushiriki katika majukwaa kama CEO Golf Tournament unaipa Vodacom Tanzania nafasi ya kukutana na viongozi wanaofanya maamuzi katika sekta ya biashara, kusikiliza mahitaji yao na kuendeleza mazungumzo kuhusu namna teknolojia inavyoweza kusaidia biashara kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Kwa Vodacom Tanzania, ushiriki katika majukwaa ya golf unaendelea kuwa sehemu ya kujenga mahusiano na viongozi wa makampuni ya biashara, kubadilishana mawazo na kuendeleza fursa za ushirikiano katika dunia ya biashara inayozidi kuunganishwa na teknolojia.

Benki ya Exim Tanzania imeungana na viongozi wa taasisi, wafanyabiashara, washirika na wadau mbalimbali katika CEO Golf Day 2026, hafla iliyofanyika Septemba 26, 2026 katika Sea Cliff Golf Club, Zanzibar, na kuwakutanisha viongozi wa biashara, wanadiplomasia na wachezaji wa gofu kutoka Tanzania na nje ya nchi.

Hafla hiyo inalenga kutumia mchezo wa gofu kama jukwaa la kuwakutanisha viongozi na wadau wa biashara kutoka Tanzania na nje ya nchi, ikiwemo Kenya, Uganda, Zambia, Malawi, Afrika Kusini na Nigeria, na hivyo kutoa nafasi kwa washiriki kutoka masoko mbalimbali kukutana kujenga mahusiano na kuendeleza mazungumzo kuhusu fursa mbalimbali.

Benki ya Exim Tanzania imeshiriki katika hafla hiyo ikiwa ni mmoja wa wadhamini, hatua inayoakisi dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na jumuiya ya wafanyabiashara na wadau mbalimbali, kuimarisha mahusiano na kujenga fursa za pamoja zinazoweza kuchangia ukuaji wa biashara nchini.

Mbali na mchezo wa gofu, hafla hiyo ilitoa nafasi kwa viongozi na washiriki kuendelea na mazungumzo na kujenga mahusiano ya kikazi. Mashindano hayo yalihusisha mchezo wa gofu wa mashimo 18, kabla ya washiriki kuhitimisha siku kwa hafla ya chakula cha jioni.

Kwa Benki ya Exim Tanzania, ushiriki huo ni sehemu ya kuendelea kuwa karibu na jumuiya ya biashara na wadau wake, wakiwemo wateja. Kwa ujumla, Dhumuni la siku hii ya kipekee ni kujenga mtandao wa kibiashara na ushirikiano wa kijamii, kuweka mazingira ambapo viongozi wa biashara na wadau wanaweza kuungana, kubadilishana mawazo na kuimarisha mahusiano nje ya mazingira ya kawaida ya kazi.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Christian Makonda, ametangaza kutoutambua mchakato wa kubadilisha jezi za timu za taifa, akisema umefanyika bila kuishirikisha Wizara licha ya maelekezo aliyoyatoa Februari 2026.

Sambamba na hatua hiyo, Waziri Makonda ameagiza kuundwa kwa kamati maalumu itakayochunguza mikataba ya wazabuni wa jezi hizo, manufaa yake kwa timu za taifa pamoja na mapato yanayotokana na mauzo yake.

Uamuzi huo umetangazwa siku mbili baada ya Waziri Makonda kukataa hadharani jezi mpya zilizoonekana zikivaliwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, akisema hazikuwa na ubora unaoendana na hadhi ya Taifa Stars.

“Hii siyo jezi ya Taifa Stars. Taifa Stars kwa ubora wake hatuwezi kuwa na jezi za kiwango cha chini hivi. Acheni kutumia picha za Naibu wangu huku ofisi yangu haina taarifa. Tuheshimiane,” alisema Waziri Makonda kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara leo, Septemba 18, 2026, uchunguzi huo unalenga kubaini iwapo mikataba iliyopo inanufaisha timu za taifa kwa kiwango kinacholingana na fedha nyingi zinazotolewa na Serikali kugharamia timu hizo.

Wizara imeeleza kuwa Februari 2026, Waziri Makonda alitoa maelekezo ya kuboresha jezi za timu za taifa ili ziakisi utambulisho wa Tanzania na kuzalisha manufaa mapana kwa nchi.

Hatua hiyo imeelezwa kuwa muhimu kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika maandalizi ya timu za taifa zinazoshiriki mashindano ya kimataifa, pamoja na Tanzania kuwa mwenyeji mwenza wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2027 (AFCON 2027).

Kamati hiyo pia itachunguza mapato yanayotokana na mauzo ya jezi na mchango wake katika kugharamia uendeshaji wa timu za taifa.

 

Na Mwandishi Wetu, Manyara

MBIO za hisani za Manyara Tanzanite Marathon 2026 zimefanyika leo katika Mji wa Babati, mkoani Manyara, huku waandaaji wakiwa na lengo la kukusanya Sh1.5 bilioni kwa ajili ya ujenzi na uwezeshaji wa wodi maalum ya kuwahudumia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.

Mbio hizo zilizoendeshwa chini ya kaulimbiu “Hatua Moja, Okoa Maisha ya Mtoto Njiti”, zimewakutanisha wananchi, wanariadha na wadau mbalimbali kutoka maeneo tofauti nchini, kwa lengo la kuunga mkono juhudi za kuboresha huduma za afya kwa watoto wachanga na watoto njiti.

Mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Mwigulu Nchemba, ambaye ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Daniel Sillo, amepongeza Mkoa wa Manyara kwa kuanzisha mbio hizo, akisema ni ubunifu unaolenga kushirikisha jamii katika kuchangia huduma za afya.

Sillo amesema Manyara Tanzanite Marathon ni mfano wa namna matukio ya michezo yanavyoweza kutumika katika kuhamasisha jamii na wadau kuchangia miradi yenye manufaa kwa wananchi, hususan katika sekta ya afya.

Amesema jitihada hizo zinapaswa kuungwa mkono na maeneo mengine nchini ili kuongeza ushiriki wa jamii katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
MBIO za hisani za Manyara Tanzanite Marathon 2026 zimefanyika leo katika Mji wa Babati, mkoani Manyara, huku waandaaji wakiwa na lengo la kukusanya Sh1.5 bilioni kwa ajili ya ujenzi na uwezeshaji wa wodi maalum ya kuwahudumia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.

Mbio hizo zilizoendeshwa chini ya kaulimbiu “Hatua Moja, Okoa Maisha ya Mtoto Njiti”, zimewakutanisha wananchi, wanariadha na wadau mbalimbali kutoka maeneo tofauti nchini, kwa lengo la kuunga mkono juhudi za kuboresha huduma za afya kwa watoto wachanga na watoto njiti.

Mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Mwigulu Nchemba, ambaye ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Daniel Sillo, amepongeza Mkoa wa Manyara kwa kuanzisha mbio hizo, akisema ni ubunifu unaolenga kushirikisha jamii katika kuchangia huduma za afya.

Sillo amesema Manyara Tanzanite Marathon ni mfano wa namna matukio ya michezo yanavyoweza kutumika katika kuhamasisha jamii na wadau kuchangia miradi yenye manufaa kwa wananchi, hususan katika sekta ya afya.
Amesema jitihada hizo zinapaswa kuungwa mkono na maeneo mengine nchini ili kuongeza ushiriki wa jamii katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Jafari Rajabu, amesema mbio hizo zina umuhimu mkubwa katika juhudi za kuokoa maisha ya watoto, huku akiwataka wananchi na wadau kuendelea kuunga mkono mipango inayolenga kuboresha huduma za afya.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, amewashukuru wadau walioshiriki katika maandalizi na utekelezaji wa mbio hizo, akisema ushirikiano wao umewezesha kufanikisha tukio hilo lenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto wanaohitaji huduma maalumu za afya.
Sendiga amesema fedha zitakazopatikana kupitia mbio hizo zitaelekezwa katika kufanikisha ujenzi na uwezeshaji wa wodi maalum kwa ajili ya kuwahudumia watoto njiti, ambao huhitaji huduma za kitaalamu na vifaa maalumu tangu wanapozaliwa.

Baadhi ya washiriki wa mbio hizo wamesema walishiriki si kwa ajili ya mazoezi na afya zao pekee, bali pia kuchangia juhudi za kuokoa maisha ya watoto wachanga na watoto njiti.

Wamesema Manyara Tanzanite Marathon imewapa fursa ya kuunganisha michezo na shughuli za kijamii, huku wakitoa wito kwa wananchi wengine kushiriki katika matukio yenye malengo ya kuboresha afya na ustawi wa jamii.

Manyara Tanzanite Marathon 2026 imeweka lengo la kukusanya Sh1.5 bilioni, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya “Hatua Moja, Okoa Maisha ya Mtoto Njiti” inayolenga kuongeza uwezo wa huduma za afya kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati mkoani Manyara.