Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MAELEFU ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na viongozi wastaafu wa Serikali zilizopita wamefika Uwanja wa Uhuru kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk.John Magufuli.

Dkt.Magufuli ambaye amefariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mnzena mkoani Dar es Salaam ambako alikuwa anapatiwa matibabu kutoka na maradhi ya moyo katika mfumo wa umeme , wananchi wa Dar es Salaam wakiongozwa na maelfu ya wananchi wamepata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kwa Dkt.Magufuli.

Uwanja wa Uhuru ambao siku zote umekuwa maarufu kwa kutoa buradani kutokana na shughuli mbalimbali za kimichezo na burudani kwa siku ya leo, kwani majonzi, vilio na simanzi ndizo ambazo zilikuwa zimetawala kutokana na msiba huo mkuwa ambao Taifa la Tanzania umelipata kwa kuondokewa na mpendwa wetu Dkt.Magufuli.

Uwanjani hapo maelfu ya wananchi walianza kujitokeza mapema alfajiri ya leo Machi 20, 2021 ambao waliokuwa wametoka maeneo mbalimbali na wote wakiwa na hamu ya kushuhudia shughuli mbalimbali za kutoa heshima zao za mwisho kwa Dk.Magufuli ambaye kwenye uongozi wake aliamini katika kuwasadia na kusikiliza wananchi wanyonge wenye changamoto mbalimbali za kimaisha.

Mwili wa Dk.Magufuli ulifikishwa Uwanja wa Uhuru saa nne asubuhi ukitokea Kanisa la St.Peters, Dar es Salaam ambako ibada maalum ya kumuaga ilifanyika kabla ya wananchi na viongozi kutoa heshima zao za mwisho katika uwanja huo.

Hata hivyo kote ambako mwili wa Dkt.Magufuli umepitishwa maelfu ya wananchi walikuwa barabarani.Wananchi walishindwa kabisa kuwa na ustahimilivu kwani asilimia kubwa ya wananchi hao walionekana wakibubujikwa na machozi kutokana na mapenzi makubwa waliyokuwa wanayo kwa Dkt.Magufuli ambaye kwenye utawala wake alihakikisha awatetea na kuwapigania.

Pamoja na hayo kabla ya wananchi wakiongozwa na viongozi kuanza kutoa heshima zao za mwisho ibada maalum ilifanyika uwanjani hapo na wakati wa ibada hiyo mengi yamezungumzwa kuhusu Dkt.Magufuli.


Endelea kufuatilia Michuzi TV na Michuzi Blog kwa ajili ya kukujuza kila kinachoendelea uwanjani Uwanja wa Uhuru ambako shughuli za kuaga mwili wa mpendwa wetu zinaendelea.

Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa na majonzi baada ra Kuwasili Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo Machi 20, 2021 katika Uwanja wa Uhuru.HABARI, JAMII
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: